Benki ya NMB imetoa shilingi milioni 42.5 kwa ajili ya kudhamini Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika katika kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu kuanzia Agosti 01 hadi Agosti 08, 2020.
Akikabidhi mfano wa hundi ya fedha hizo Julai 27, 20202 kwa Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi, Bw. Sospeter Magese amesema katika mchango huo, NMB pia imetoa fulana 300 ambazo zitatumika katika maonesho hayo.
Bw. Magese amesema NMB imekuwa ikidhamini maonesho haya tangu mwaka wa 2018 yalipoadhimishwa kwa mara kwanza mkoani Simiyu ambapo mpaka sasa benki hiyo imeshatoa shilingi 100.
“Pamoja na kudhamini maonesho ya nanenane Benki ya NMB imekuwa ifanya kazi na katika maeneo mengi katika sekta ya elimu pamoja na kilimo; katika kilimo ndani ya miaka miwili tumeweza kufungua akaunti 500,000 lakini kati ya hizo akaunti 86,000 ni za wakulima wa pamba wa mkoa wa Simiyu,” alisema Magese.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa mkoa wilaya ya Bariadi, Mku wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ameishukuru Benki ya NMB kwa namna inavyojitoa kusaidia mambo mbalimbali katika mkoa wa Simiyu ikiwemo katika sekta ya elimu pamoja na kilimo huku akiwahakikishia kuwa serikali iko tayari kushirikiana na benki hiyo kila itakapohitaji.
Katika hatua nyingine Kiswaga ametoa wito kwa wananchi wa mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na maeneo yote nchini kujitokeza kwa wingi kujionea maonesho ya kilimo nanenaneyanayofanyika Kitaifa katika kanda ya ziwa Mashariki ili kuona fursa mbalimbali pamoja na teknolojia rahisi zinazotumika katika sekta ya kilimo.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/07/nmb-yatoa-milioni-425-kuchangia.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa