Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa rai kwa Benki ya NMB kuja na utaratibu utakaowasaidia watumishi wa Umma ambao wamefikia kiwango cha mwisho cha kukopa kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) pale wanapobakia na moja ya tatu ya mishahara yao ili waweze kupata msaada wakati wa dharura.
Mtaka ameyasema Mjini Bariadi hayo Septemba 30, 2020 katika Warsha maalum ya Teachers’ Day iliyoandaliwa na Benki hiyo na kuwakutanisha walimu wakuu, wakuu wa shule, waratibu wa elimu, maafisa elimu na wadhibiti ubora wa mkoa wa Simiyu.
“Watumishi wengi wamekuwa wanaangukia mikononi mwa wakopeshaji binafsi wenye riba kubwa kutokana na kushindwa kukopesheka baada ya mishahara yao kutoruhusu makato ya mikopo inapofikia moja ya tatu ya mishahara yao kwa mujibu wa BOT, wanapopata dharura kwenye familia zao inawalazimu kukopa huko, benki kubwa kama NMB mje na ‘package’ ya kusaidia hili,” alisema Mtaka
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa