Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara(NBC) ,Theobald Sabi amewahakikishia wakazi wa Bariadi Mkoani Simiyu kuwa Benki hiyo itafungua tawi Mjini Bariadi ili kusogeza huduma karibu na wananchi.
Sabi ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Wakala Mkubwa (Super Agent) Mjini Bariadi, Agosti 07, 2018.
Amasema Wilaya ya Bariadi na Mkoa wa Simiyu ina wateja wengi wa NBC lakini huduma zilikuwa mbali hivyo, kufunguliwa kwa wakala mkubwa (SUPER AGENT) ni sehemu ya mpango wa kupeleka karibu huduma kwa wateja wao.
“Hapa Bariadi tuna wateja wengi lakini huduma zilikuwa zinapatikana mbali, hivyo kufunguliwa kwa wakala huu ni kutawasaidia wateja wetu kupata huduma karibu na tutaendelea kuongea na wananchi ili tuweze kupata tawi la NBC, ni nia yetu hivi karibuni kuongeza tawi hapa Bariadi” alisema .
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kufunguliwa kwa Wakala Mkubwa wa NBC Bariadi kumekuja katika wakati muafaka ambapo utaweza kupima mzunguko wa fedha mjini Bariadi na kuwa njia ya kwenda kwenye kufungua Tawi kamili la NBC.
Amesema Mkoa wa Simiyu ni mkoa mpya unaojengwa kiuchumi hivyo ikiwa benki hiyo ikijipanga vizuri Wakala huo uliofunguliwa utafanya biashara kwa kuwa wakazi wa mkoa wa Simiyu ni wafayabiashara wazuri wa mazao mbalimbali pamoja na mifugo.
“Mkoa wa Simiyu ni mkoa wenye Uchumi mzuri tunao uwezo wa kuzungusha zaidi ya Bilioni 100 wakati wa mavuno ya pamba, benki ikijipanga vizuri na ikapata msimamizi mzuri wa wakala anayefahamu biashara ya benki mtafanya biashara, Wanyantuzu ni wafanyabiashara hakuna Mnyantuzu mcheza pulu” alisema
Naye Mfanyabiashara wa Mjini Bariadi, Bw. John Sabo ameshukuru uanzishwaji wa Wakala huo ambao utawapunguzia adha ya kufuata huduma mikoa ya Mwanza na Shinyanga na kuabainisha kuwa Wakala tu hautoshi, hivyo wafanyabiashara wengi wenye akaunti NBC wanaomba Benki ya NBC kufungua Tawi kamili Mkoani Simiyu.
MWISHO.
KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/08/benki-ya-nbc-yaahidi-kufungua-tawi.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa