• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Naibu Waziri wa Fedha: Wanafunzi wa Kidato cha Nne, Darasa la Saba Yatumieni Maarifa Mliyoyapata kuongeza ufaulu

Posted on: June 24th, 2018

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amewaasa wanafunzi wa darasa la saba na Kidato cha nne  katika shule zote za msingi na sekondari mkoani Simiyu waliokuwa katika kambi za kitaaluma mkoani humo kwa takribani siku 21 kuyatumia vema mafunzo waliyopata katika kambi hizo, kama msingi wa safari yao ya ufaulu katika mitihani ya Kitaifa.

Dkt Kijaji ametoa ushauri huo kwa nyakati tofauti katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Halmashauri ya wilaya ya Maswa wakati akifunga kambi za  kitaaluma kama mgeni rasmi akiwa kwenye ziara pamoja na viongozi wa Halmashauri na CCM Wilaya ya Kondoa iliyolenga kujifunza uendeshaji wa kambi za kitaaluma kwa wanafunzi wa darasa la saba na kidato cha nne na utekelezaji wa sera ya Tanzania ya Viwanda. na Serikali mkoani Simiyu.

“Watoto wangu hii fursa mliyoipata ni muhimu sana kwenu itumieni vizuri, siku 21 mlizokaa kwenye kambi za kitaaluma katika mkoa mzima ni zaidi ya dhahabu kwenye maisha yenu, kihifadhini hiki mlichokipata mnapoenda nyumba nendeni mkayafanyie kazi yote mliyoyapata, hapa ndiyo ukombozi wa kifikra umeanza” alisema Dkt. Kijaji.

Dkt Kijaji pia ametumia hadhira hiyo kuwakumbusha wazazi, walimu pamoja na watendaji wa Serikali kuwa dhana ya uchumi wa viwanda haiwezi kufikiwa bila ya elimu iliyo  hivyo juhudi za pamoja zinahitaji kuhakikisha kuwa wanafunzi wanasoma vizuri kwa ajili ya kuandaliwa kuwa wataalam wa baadaye.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walimu, wazazi na wanafunzi wameshukuru uongozi wa Mkoa na wilaya kuanzisha utaratibu wa kambi za kitaaluma ambao wamekiri kuwa umesaidia kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa mapya hivyo wakaomba utaratibu huu  uendelee ili kuwaandaa vema wanafunzi wa madarasa ya mitihani na kuongeza ufaulu.

“Kambi hii ni nzuri sana kwa sababu walimu wanatufundisha vizuri na tunaelewa, tumepata maarifa ya kutosha yatakayotusaidia,  nina uhakika mtihani wa kumaliza darasa la saba tutafanya vizuri sana, naomba hata wadogo zetu nao wakaweke pia kambi,”alisema Tumain Stephano mwanafunzi kutoka Sima B Mjini Bariadi.

“Tunawashukuru viongozi kwa kutuanzishia kambi hizi, zimetusaidia kukutana na wenzetu kujifunza, kama tungekuwa nyumbani wakati wote wa likizo tungekuwa hatusomi kama tunavyosoma hapa na tusingepata haya tuliyoyapata, naomba kambi ziendelee” Maria Patrick kutoka Shule ya Msingi Sima A.

“Katika kambi hizi zimeongeza ushirikiano katika ya walimu na wanafunzi wa shule zilizokutanishwa pamoja, pia tulikuwa na mitihani ambayo imewasaidia wanafunzi kuongeza bidii wanapoona wamefanya vibaya hali iliyochangia kuongeza nguvu ya kujisomea na kuboresha hali ya ufaulu kwa watoto, tunaomba ziendelee” Mwalimu Aloyce Masejo,”

Akizungumza  kwa niaba ya wazazi Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Sima A, Bw. Bashiru Kishama amesema Kambi za kitaaluma zimechangia kuimarisha umoja na ushirikiano kati ya walimu na wazazi wa Shule zilizoweka wanafunzi wao pamoja, huku akibainisha kuwa walichojifunza wanafunzi kitawasaidia kufanya vizuri katika mitihani yao hivyo akaomba kambi hizi ziwe endelevu.

Wazazi wilayani Maswa walioshiriki zoezi la kufunga kambi za kitaaluma wilayani Maswa wamesema wataendelea kuunga mkono suala hilo  kwa kuwa wameona faida yake huku wanafunzi wakiwashukuru viongozi wa Serikali kwa kuanzisha kambi hizo na kuomba zifanyike tena mwezi Septemba na ziwe endelevu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Mhe. Gasper Mwenda amepongeza viongozi wa mkoa wa Simiyu kwa namna wanavyofanya kazi kwa ushirikiano na kuzungumza lugha moja katika suala la maendeleo ya wananchi jambo ambalo ameahidi kuwa wamejifunza na wataenda kulifanyia kazi katika wilaya yao ya Kondoa.,

Katika katika zoezi la kufunga kambi wilayani Maswa viongozi mbalimbali wametoa michango ya fedha taslimu na ahadi ya vitu na fedha kwa ajili maandalizi ya kambi za Kitaalum zitakazoanza mwezi Septemba kwa kidato cha nne ambapo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametoa shilingi 500,000/= , Mbunge wa Maswa Mashariki na Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanslaus Nyongo shilingi 500,000/= na kuahidi zawadi mbalimbali kwa wanafunzi watakaokuwa katika nafasi kumi bora Kitaifa na Shule kumi bora

Jumla ya wanafunzi 35,213 wa Shule za msingi na wanafunzi 7,169  wameshiriki katika kambi za Kitaaluma kwa Wilaya zote za Mkoa wa Simiyu.

Wanafunzi wa darasa la saba katika Shule za Msingi Sima A na B wakimpungia mikono Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji wakati alipofika shuleni hapo kuzungumza nao kabla ya kufunga kambi za kitaaluma zilizofanyika kwa muda wa siku 21 katika kipindi cha likizo mwezi Juni.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Julius Nestory akitoa taarifa ya maendeleo yakambi za kitalaluma mkoani humokwa Naibu Waziri wa Fedh na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akikabidhi fedha taslimu shilingi lakini tano kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajaili ya kuunga mkono maandalizi ya kambi za kitaaluma zitakazoanza mwezi Septemba, 2018 Mkoani Simiyu, wakati akifunga kambi hizo zilifanyika kwa siku 21 mwezi huu Juni, mkoani humo

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na viongozi, wazazi na wanafunzi wa baadhi ya Shule za Msingi na sekondari wakati wa kufunga kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa darasa la saba na kidato cha nne Mkoani Simiyu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Mhe. Gasper Mwenda akizungumza na wanafunzi wa Shule za Msingi Sima A na B mjini Bariadi wakati wa hafla ya kufunga kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa darasa la saba na kidato cha nne Mkoani Simiyu, iliyoongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji.

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Sima A mjini Bariadi akitoa maoni yake juu ya kambi za Kitaaluma katika hafla ya kufunga kambi hizo iliyoongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashati Kijaji mkoani Simiyu.

Mwalimu aliyekuwa mlezi wa wananfunzi kambi a Shule ya Msingi Sima B mjini Bariadi akitoa maelezo ya maendeleo ya kambi ya kitaaluma mbele ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashatu Kijaji  wakati wa kufunga kambi hizo mkoani Simiyu.

Kalebu Saimon mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Dekapoli wilayani Maswa akitoa maoni yake juu ya kambi za Kitaaluma katika zoezi la kufunga kambi hizo lililoongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashati Kijaji mkoani Simiyu.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, wakati wakiwa kwenye zoezi la kufunga kambi za kitaaluma mkoani Simiyu.


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa