Bariadi,
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete ameridhishwa na Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) inayotekelezwa ndani ya Mkoa wa Simiyu.
Naibu Waziri Kikwete ametoa pongezi hizo 14 Septemba 2023 alipozungumza na Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika ziara yake yenye lengo la kukagua Miradi mbalimbali ya TASAF Mkoani humo.
Amesema miradi ya TASAF ni tofauti na miradi mingine ya serikali kwa sababu inaonekana kwa macho na utekelezaji wake unawagusa wananchi waishio vijijini moja kwa moja.
Amesema Utekelezaji wa miradi ya kupunguza Umaskini (TPRP) kupitia Mpango wa Kunusu Kaya Maskini, umefanikiwa kutokana na mipango mizuri ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia ambapo zaidi ya Bil. 9.2 zimetolewa katika mkoa wa Simiyu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.
‘’TASAF wana Uwezo wa kuzisimamia hizo fedha, kama hakuna uwezo wa kuzisimamia, tutaishia kugombana tu, tunachotaka tukileta fedha tuone thamani halisi ya fedha hizo…hivi ndivyo miradi inavyotakiwa kufanyika’’ amesema Ridhiwan.
Amezitaka Halmashauri kujifunza kwenye miradi ya TASAF ambayo imekuwa ikitekelezwa kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi na inatekelezwa na watu wanaotaka matokeo yanayooneka.
GCO,
Simiyu RS
14 Septemba 2023.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa