• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Naibu Waziri Silinde Atoa Miezi Miwili Bariadi, Itilima Kukamilisha Mabweni

Posted on: March 5th, 2021

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ametoa miezi miwili kuanzia sasa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Itilima kukamilisha ujenzi wa mabweni katika  shule ya sekondari Bariadi, Nyasosi na Itilima ili wanafunzi waliokusudiwa kukaa katika mabweni hapo wapate huduma tarajiwa kwa wakati.

Silinde ametoa agizo hilo wakati alipotembelea shule hizo wakati wa ziara yake Machi 05, 2021 Mkoani Simiyu yenye lengo la kukagua ujenzi wa majengo ya miundombinu ya elimu ikiwemo mabweni, mabwalo na vyumba vya madarasa.

 

Amesema Serikali haitatoa fedha nyingine kukamilisha mabweni, mabwalo na madarasa ambayo bado hayajakamilika na haitakubali yabaki magofu  hivyo ni jukumu la Halmashauri husika kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha majengo hayo ili wanafunzi waliokusudiwa kutumia wapate haki yao.

“Nimeridhishwa na kiwango cha ujenzi wa madarasa na thamani ya fedha inaonekana ninawapongeza sana, kuhusu mabweni mhakikishe yanakamilika na ninaahidi kurudi tena hapa mwezi Mei kuja kukagua kuona namna mlivyotekeleza, yasipokamilika ninawaambia wazi nitawavua madaraka wakuu wa shule na maafisa Elimu sekondari,” alisema Silinde.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi.Elizabeth Gumbo ameahidi kukamilisha ujenzi wa bweni shule ya sekondari Itilima ifikapo Aprili 30, 2021 huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Bw. James John akiahidi kukamilisha bweni la Shule ya sekondari Nyasosi tarehe hiyo hiyo na Mkurugenzi wa Mji wa Bariadi,Melkizedeck Humbe ameahidi kukamilisha ujenzi Mei 15, 2021.

Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi amesema shule ya Sekondari Itilima ilipokea shilingi milioni 80 kwa ajili ya ujnezi wa bweni ambapo amebainsha kuwa baadhi ya sababu zilizopelekea mradi huo kutokamilika kwa fedha hiyo ni pamoja na aina ya udongo uliopo katika eneo la Ujenzi kuhitaji msingi mrefu na imara uliotumia fedha nyingi tofauti na makadirio pamoja na kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi.

Pamoja na changamoto hizo Kilangi amesema Serikali wilayani humo itahakikisha Bweni la Shule ya Sekondari Itilima linakamilika kwa wakati ili kuwawezesha wanafunzi kupata huduma iliyokusudiwa kwao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya  Bariadi Mhe. Festo Kiswaga amewaagiza wataalam wa Halmashauri zote mbili za Wilaya ya Bariadi kuhakikisha wanakamilisha majengo yote yaliyoletewa fedha na serikali huku akimhakikishia Naibu Waziri kuwa mabweni ya Bariadi sekondari na Nyasosi sekondari yatakamilika kwa wakati.

Katika hatua nyingine Kiswaga amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya hiyo kumpelekea taarufa ya fedha zote za miradi zinazoingia ili kamati ya ulinzi na usalama iweze kujua na kuweka utaratibu wa kuzisimamia na kuhakikisha zinatekeleza miradi kulingana na maelekezo ya Serikali.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2021/03/naibu-waziri-silinde-atoa-miezi-miwili.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa