• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Naibu Waziri Ndugulile Ahimiza Wajawazito Kujifungulia Katika Vituo vya Afya Kupunguza Vifo Vitokanavyo na Uzazi

Posted on: July 23rd, 2018

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ametoa wito  kwa akina mama wajawazito kuona umuhimu wa kuhudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo Julai 22,2018 katika nyakati tofauti wakati akiwa katika ziara yake katika Wilaya ya Bariadi na Itilima mkoani Simiyu.

Amesema Serikali imefanya jitihada kubwa katika kujenga vituo vya kutolea huduma za afya, majengo ya upasuaji na wodi za wazazi hivyo ni vema wananchi wakatumia vituo hivyo ili idadi ya wanawake wanaojifungulia majumbani ipungue na idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi pia iendelee kupungua.

“Huduma tumewasogezea karibu mzitumie, hususani wakina mama wajawazito, ujauzito siyo ugonjwa na wala mwanamke hatakiwi kufariki sababu ya ujauzito, tuhakikishe wakina mama wanahudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma, tunataka vifo vya akina mama na watoto viwe historia” alisema Dk. Ndugulile.

Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akisoma taarifa ya Mkoa kwa Naibu waziri,  amesema idadi ya akina mama wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya imeongezeka kutoka asilimia 54 mwaka 2016 na kufikia asilimia 81 mwaka 2017, huku idadi ya vifo ikiongezeka kufikia vifo 48 kutokana na sababu mbalimbali.

Kutokana na takwimu kuonesha idadi ya vifo kuongezeka Naibu Waziri Dkt. Ndugulile  amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa na idara ya Afya mkoa wa Simiyu kuangalia chanzo cha ongezeko hilo na kuchukua hatua stahiki dhidi ya vifo hivyo ili kukomesha kabisa vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi.

Aidha, Dkt. Ndugulile ameuomba uongozi wa mkoa wa Simiyu kufuatilia watu zaidi ya 10000 walioonekana kuacha kutumia dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVs) ili kuweza kukabiliana na maambukizi mapya.

Katika hatua nyingine Dkt. Ndugulile ametoa wito kwa viongozi na jamii mkoani Simiyu kuendelea kupambana na mimba za utotoni kwa kuweka mikakati ya kuhakikisha watoto wote wa kike wanakwenda shule na kuwachukulia hatua kali wale watakaobainika kuwapa wanafunzi mimba kwani mimba za utotoni pia zimekuwa chanzo cha ongezeko la vifo vya akina mama wajawazito.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo imeendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wanaume wanaobainika kuwapa mimba wanafunzi ambapo amebainisha kuwa hadi sasa ni takribani watu 9 wameshachukuliwa hatua.

Kuhusu suala la VVU Mhe. Mtaka amesema Serikali mkoani humo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuwahimiza wananchi kupima VVU huku akibainisha kuwa idara ya afya itafanya mpango wa kuweka huduma za ushauri na kupima VVU pamoja na magonjwa yasiyoambukiza katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane kwa kuwa itahusisha watu kutoka maeneo mbalimbali.

Mhe. Dkt. Ndugulile akiwa wilaya ya Bariadi na Itilima ametembelea Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD)la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Jengo la Kituo cha Afya Ikindilo, Wodi ya Wazazi katika zahanati ya Nangale na Migato ambapo amesema ameridhishwa na kazi ya ujenzi iliyofanyika na thamani ya fedha iliyotumika

Akiwa katika wilaya ya Itilima ameahidi kulifanyia kazi ombi la Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga, Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi  na Diwani wa Kata ya Migato Mhe. Mbuga Ntobi la kujenga kituo cha Afya katika Kata ya Migato kwa kulipeleka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ili wananchi waweze kusogezewa huduma jirani.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:- https://simiyuregion.blogspot.com/2018/07/naibu-waziri-ahimiza-wakina-mama.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa