• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Naibu Waziri Kilimo Awaasa Wakulima Kuzingatia Matumizi ya Mbolea Kuongeza Mavuno, Tija kwenye Uzalishaji

Posted on: March 7th, 2019

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba ametoa wito kwa wakulima Mkoani Simiyu kuondokana na dhana potofu kuwa matumizi ya mbolea yanazeesha ardhi  badala yake wazingatie matumizi sahihi ya mbolea katika  kilimo ili kuongeza mavuno, tija na uzalishaji katika kilimo.

Mhe. Mgumba ameyasema hayo Machi 06, 2019 wakati akizungumza na wananchi wilayani Itilima Mkoani Simiyu, katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Bukingwaminzi kata ya Zagayu wilayani humo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu.

Ameongeza kuwa siyo kweli kwamba matumizi ya mbolea yanazeesha ardhi badala yake mbolea inasaidia kutibu ardhi na kupelekea wakulima kuongeza mavuno na tija katika uzalishaji wa mazao na kuwawezesha kushindana katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

“Nimeambiwa hamtaki kutumia mbolea kwa madai kwamba mkitumia mbolea inazeesha ardhi siyo kweli, mbolea hizi haziharibu ardhi yetu bali zinakwenda kutibu ardhi;ndiyo maana watu wa Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya , Songwe, Rukwa na Katavi wanaongoza kwa kuzalisha mahindi nchini wenzetu ni wajanja wanatumia Mbolea”alisema

Akizungumzia suala la viuatilifu Mgumba amewahakikishia wakulima wa zao la pamba mkoani Simiyu kuwa tayari bodi ya pamba imeshatoa chupa 1000 za viuatilifu/viuadudu ambapo kila wilaya itapata chupa 200.

Katika hatua nyingine Mhe. Naibu Waziri amezungumzia suala la bei ya pamba ambapo amesema Serikali inaendelea kuandaa mazingira wezeshi kwa wanunuzi wa pamba wa ndani na nje ya nchi kununua pamba ya wakulima kwa bei nzuri na kubainisha kuwa utaratibu utakaotumika ni wa soko huria.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga pamoja na kuomba pamba iuzwe kwa bei ya soko huria na kuongezewa viuatilifu, ameomba maghala ya kuhifadhia pamba yajengwe kupitia sehemu ya fedha inayotolewa na wakulima katika Vyama vyao vya Ushirika ili pamba ihifadhiwe vizuri na tija ionekane.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi amesema jitihada zinaendelea kufanyika kuwahamasha wakulima wote wa pamba kujiunga na vyama vya ushirika ambapo amesema hadi sasa ni wakulima 11,700  kati ya  38,910 wako katika vyama vya ushirika vipavyo 56.

Nao baadhi ya wananchi waliopata nafasi ya kuwasilisha maombi na kero zao kwa Naibu Waziri wa Kilimo wameomba viuatilifu/viuadudu vilivyotolewa na bodi ya pamba viwafikie wakulima  kwa wakati.

Naibu Waziri Mgumba yuko mkoani Simiyu katika ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua shughuli za kilimo na ushirika zinavyoendelea na kukagua shughuli za miradi ya umwagiliaji akiwa Wilayani Itilima amepata nafasi ya kuzugumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI OFUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/03/naibu-waziri-kilimo-awaasa-wakulima.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa