• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Naibu Waziri Ikupa awaomba Wadau kuwasaidia Walemavu Vifaa Saidizi

Posted on: February 28th, 2019

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu nayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa ametoa wito kwa wadau kuendelea kutoa msaada wa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu kwa kuwa hili ni hitaji endelevu kwa watu hao.

Mhe. Ikupa ameyasema hayo jana Februari 27, 2019 wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Serikali wilayani Busega mkoani Simiyu wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo.

Amewashukuru viongozi wa Wilaya ya Busega kwa namna inavyowasaidia watu wenye ulemavu katika kuwapatia vifaa saidizi huku akibainisha kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuwatafutia na kuwapatia watu wenye ulemavu vifaa hivyo kwa kadri vitakavyopatikana.

“Napenda kuwashukuru viongozi wa Busega kwa namna wanavyowasaidia watu wenye ulemavu kupata vifaa saidizi kama fimbo nyeupe kwa wasioona, baiskeli na viungo bandia kwa walemavu wa viungo, mafuta kwa wenye ualbino, lakini niwaombe wadau waendelee kuwasaidia kwa kuwa hili ni hitaji endelevu katika kuishi kwao.” alisema Mhe. Ikupa.

Katika hatua nyingine Mhe. Naibu Waziri amesisitiza Kamati za watu wenye ulemavu kupewa miongozo ya namna ya kuziendesha kamati hizo, ili ziweze kutimiza majukumu yake ipasavyo na kuzitaka kutoa taarifa kuhusu fursa na masuala mbalimbali yanayowahusu walemavu katika maeneo yao.

Vile vile Mhe. Ikupa amesema Serikali inatarajia kuanzisha mfuko wa watu wenye ulemavu ambao utakuwa ukishughulikia masuala mbalimbali ya watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku kwa vyama vya walemavu.

Akitoa taarifa Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera, amesema Serikali wilayani imetoa baiskeli 17 kwa watu wenye ulemavu wa viungo, zaidi ya fimbo nyeupe 50 kwa wasioona, mafuta kwa watu wenye ualbino na Halmashauri imeandaa mpango maalum wa Mfuko wa Bima ya Afya(CHF) iliyoboreshwa kwa ajili ya huduma za afya kwa walemavu.

Kwa upande wao watu wenye ulemavu wameiomba Serikali na wadau kuendelea kuwapa msaada wa vifaa saidizi , kupewa elimu ya kuunda vikundi na kuandaa maandiko ya miradi na kutoa semina elekezi kwa kamati za watu wenye ulemavu.

“Mahitaji ya walemavu bado ni makubwa tunaomba wadau mbalimbali waendelee kutukumbuka kutupa msaada wa vifaa saidizi kama fimbo nyeupe kwa wasioona, viungo bandia na baiskeli kwa walemavu wa viungo lakini na mafuta kwa wenzetu wenye ualbino” alisema Katibu wa  SHIVYAWATA Wilaya ya Busega, Makasi Egonjo.

“Tunaishukuru Serikali kwa kutusaidia kwenye mahitaji yetu mengi lakini tunaendelea kuomba wasichoke kutusaidia, tunaomba maafisa ustawi wa jamii wawafikie watu wenye ulemavu mpaka waliopo vijijini ili tuwe na elimu kuhusu mambo yanayotuhusu na fursa za mikopo na ujasiriamali” alisema Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona, John Daniel

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amemhakikishia Naiba waziri Ikupa kuwa Mkoa wa Simiyu utaendelea kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa katika ziara yake na kuhakikisha walemavu wanashirikishwa na kufikiwa katika fursa mbalimbali.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa amehitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani Simiyu Febrauari 27, 2019 ambapo alipata nafasi ya kuzungumza na  viongozi wa serikali, watu wenye ulemavu na kukagua mradi wa kitalu nyumba katika Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu.

MWISHO


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa, akizungumza na viongozi wa Serikali na watu wenye ulemavu  wilayani Busega, wakati wa ziara yake Wilayani humo Februari 27, 2019.

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:- https://simiyuregion.blogspot.com/2019/02/naibu-waziri-ikupa-awaomba-wadau.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa