• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Naibu Waziri Ikupa Apongeza Ubunifu wa Kambi za Kitaaluma Simiyu

Posted on: October 30th, 2019

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, amefunga rasmi kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne Mkoani Simiyu, ambapo amewapongeza viongozi wa mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka kwa ubunifu huo ambao utawasaidia wanafunzi hao kufanya vizuri katika mitihani yao.

Naibu Waziri Ikupa ameyasema hayo Oktoba 30, 2019 wakati wa kuhitimisha kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha nne ambayo imefanyika kwa muda wa siku 60 katika Shule ya sekondari Simiyu na Chuo cha Ualimu Bariadi Mjini Bariadi, kwa lengo la kuwaandaa na mtihani wa Taifa unaotarajia kufanyika kuanzia Novemba 04, 2014.

“Nampongeza Mkuu wa Mkoa kwa ubunifu mkubwa wa kuandaa kambi hizi kwani, naamini wanafunzi mmejifunza mambo mengi na mtafanya vizuri katika mtihani wenu, ningeshauri watu wengine waige jambo hili, niwakumbushe wanafunzi mtakaoanza mtihani wenu Novemba 4, 2019, kumuomba Mungu ili awaongoze kipindi chote cha mitihani,” alisema Ikupa.

 Aidha, Ikupa amesema Serikali imeendelea kuboresha sekta ya elimu nchi kwa kuongeza bajeti katika shule, kujenga madarasa, na anaamini kuwa itaendelea kutatua changamoto ya walimu katika mkoa wa Simiyu, na nchini kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema uongozi wa Mkoa, walimu, wazazi na wadau wote wa elimu mkoani humo wamefanya uwekezaji mkubwa kwa wanafunzi wote waliokuwa katika kambi za kitaaluma na kupitia kazi nzuri iliyofanywa na walimu anaamini kwamba watafanya vizuri katika mtihani wa Taifa utakaoanza Novemba 4, 2019.

Ameongeza Serikali mkoani Simiyu itaendelea kuwapa motisha walimu, wanafunzi na shule zote zitakazofanya vizuri katika mitihani ya Kitaifa, huku akiahidi kuwalinda walimu wote, ambapo ameahidi  kuwa kuanzia Desemba Mosi, 2019 viongozi wa mkoa watawatembelea walimu katika Halmashauri zote na kuzungumza nao.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amewaomba wadau kuendelea kuunga mkono kambi hizi ili waweze kutimiza ndoto zao huku akibainisha kuwa kupitia kambi hizo watapatikana viongozi mahiri wa baadaye.

Katibu Mkuu, Chama cha Walimu Tanzania, Deus Seif amesema walimu wana imani na Serikali na wameamua kufanya kazi yao kwa bidii na wanaiomba Serikali kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kupandishwa madaraja na mishahara kwa wakati na malipo ya fedha za likizo na malimbikizo ya mishahara.

Naye Afisa Elimu wa Mkoa, Mwl. Ernest Hinju amesema tangu kambi hizi zianze mwaka 2016 zimesaidia kuongeza kiwango cha ufaulu katika matokeo ya darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita, ambapo kwa kidato cha nne  mwaka 2017 ufaulu ulikuwa 70.68% na mwaka 2019, ufaulu umekuwa 86.46%.

Naye Diana Boniphace mwanafunzi kutoka Shule ya sekondari Kidinda amesema, “kupitia kambi hii wanafunzi tumejifunza mambo mengi kupitia kwa walimu mahiri na kiwango cha ufaulu kimeongezeka tofauti na tulivyoingia hivyo tunaahidi kuwa tutafanya vizuri katika mtihani wa Taifa tutakaoanza Novemba 04, 2019.”

Kambi ya Kitaaluma iliyohitimishwa Oktoba 30, 2019 ilihusisha wanafunzi 1512 ambao walikuwa na ufaulu hafifu(daraja sifuri), wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa Mkoa(Mock) na wanafunzi kutoka shule  zenye wanafunzi chini ya 30 na wamekaa kambini siku 60.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/10/naibu-waziri-ikupa-apongeza-ubunifu-wa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa