• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Naibu Waziri Aagiza Halmashauri Kutambua Maeneo Yasiyoendelezwa na Yasiyomilikiwa Kihalali

Posted on: August 24th, 2017

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb), ameziagiza Halmashauri nchini, kuyatambua na kuyatolea taarifa  maeneo yanayohodhiwa na watu bila kuendelezwa na yale ambayo hayakupatikana kihalali ili Wizara iweze kuchukua hatua stahiki.

Naibu Waziri huyo ameyasema hayo alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali, kisha Halmashauri ya Busega Mkoani Simiyu kuanza ujenzi wa mradi wa maji katika eneo hilo utakaonufaisha vijiji vinne vya kata ya Lamadi.

Mhe.Mabula amesema Halmashauri zinapaswa kutambua maeneo yasiyoendelezwa na yanayomilikiwa kinyume cha sheria na kuwasilisha taarifa katika Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili yaweze kuyarejesha kwa wananchi na kupangiwa matumizi mengine yenye manufaa zaidi kwa jamii.

“Maeneo yote yaliyohodhiwa ambayo hayajaendelezwa na ambayo pengine hayakupatikana kihalali, ni jukumu la Halmashauri kuyatambua na  kuleta taarifa zake Wizarani ili Wizara iweze kuchukua hatua ya kuweza kuyarudisha katika matumizi kwa Umma na yaweze kufaidisha watu wengi zaidi badala ya mtu mmoja” amesema Naibu Waziri Angelina Mabula

Aidha,Naibu Waziri Mabula amebainisha sababu zilizopelekea Mwekezaji Hermati Pateli kufutiwa hati ya eneo hilo na Serikali kuwa ni udanganyifu wa Uraia pamoja na upatikanaji wa hati ambao haukuzingatia sheria na taratibu za nchi.

Naibu Waziri huyo amesema eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji huyo isivyo halali ambalo limefutiwa hati miliki limegawanyika katika ploti mbili, ploti Namba 01 na Namba 02 Block C  lenye ukubwa wa hekta 7.62 na Block Namba 03 C hekta 5.45.

Akitoa maelezo kwa  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb), Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Maji wa Lamadi kutoka Kampuni ya EAU Consult, Baraka Felix amesema Tanki la Maji litakalojengwa katika eneo hilo litakuwa na uwezo wa kuzalisha mita za ujazo 3000 kwa siku.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya amesema Mradi wa  Maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo hilo utawanufaisha wananchi wa Vijiji Vinne vya Kalago, Lamadi, Lukungu na Mwabayanda.

Mradi huu wa maji unaojengwa katika eneo hili lililokuwa linamilikiwa isivyo halali na Mwekezaji Pateli, utagharimu kiasi cha Yuro milioni 2.8, na unatarajiwa kukamilika ifikapo Mei, 2019.

Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) alipotembelea kuona Ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Maji Lamadi itakayosimamia mradi wa maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali .



Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa