• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Naibu Spika Dkt. Tulia Mgeni Rasmi Simiyu Festival 2018

Posted on: June 28th, 2018

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.  Dkt. Tulia Ackson anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio kubwa linalojulikana kwa jina la Simiyu Jambo Festival, ambalo linatarajiwa kufanyika Julai 8 mwaka huu katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, ambapo kwa mwaka huu 2018 linafanyika kwa mara ya pili

Tukio  hilo ambalo linafanyika kwa mara ya pili , limebeba vipengele vikuu vinne vya mashindano ambavyo ni mashindano ya mbio za baiskeli, ngoma za asili( wagika na wagalu), mbio fupi kilomita 10 kwa wanaume na wnawake, mbio za uwanjani kwa watoto na uandishi wa insha ambapo kauli mbio yake ni Familia Yangu, Afya Yangu, Furaha Yangu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati ya uzinduzi wa tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema kuwa tukio hilo, linalengo la kukuza vipaji kwa vijana wa Mkoa wa Simiyu na kutangaza tamaduni za kabila la Kisukuma na kwamba litahusisha wananchi wote kutoka mikoa mbalimbali.

“Tutakuwa na mashindano ya mbio za baiskeli kilomita 150 wanaume, kilomita 100 wanawake, kilomita 11 watu wenye ulemavu,  mbio fupi za kilomita 10 wanaume na wanawake, mbio za watoto za uwanjani, uandishi wa insha kwa wanafunzi na  zaidi ya shilingi milioni 22 zitashindaniwa nitoe wito kwa Watanzania wote hususani vijana kuchangamkia fursa hii” alisema Mtaka

“Hii ni fursa pia kwa Wanasimiyu ambao ni wenyeji, sisi tunasema mbio za barabarani na uwanjani ni biashara , mashindano ya baiskeli ni biashara lakini kikubwa zaidi hili ni tukio ambalo litautangaza utamaduni wa Wasukuma wenye mvuto sana ambapo makundi mawili ya Wagika na Wagalu watacheza ngoma za asili na fisi na chatu, nitoe wito kwa watu wote kuja kuona haya” alisisitiza

Mtaka amesema ushiriki katika mashindano ya mbio za baiskeli, ngoma za asili na uandishi wa insha ni bure isipokuwa mbio za kilomita 10 kwa wanawake na wanaume ambazo washiriki watatakiwa kulipa gharama ya shilingi 5,000/= kwa ajili ya usajili.

Naye Joseph Paulo Mwenyekiti chama cha Baskeli Mkoa wa Simiyu amesema kuwa uongozi mzima wa chama chao tayari wamejipanga ipasavyo kupokea na kusajili washiriki ambao watakuwa tayari kushiriki mashindano hayo ya Baiskeli kwa wanawake na wanaume.

Dkt. Amir Ibrahimu mwakilishi wa shirika la UNFPA, Mkoa wa Simiyu amesema shirika hilo limeamua kuwa ni moja ya wadhamini wa Simiyu Jambo Festival waweze kufikisha elimu wananchi wa Simiyu na jamii yote kwa ujumla itakayowasaidia kuona umuhimu wa uzazi wa mpango, kupinga mimba za utotoni na kuhamasika wakina mama wajawazito kujifungua kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua.

Aidha Akizungumzia zawadi kwa washindi watakao shiriki mashindano mbalimbali katika tukio hili la Simiyu Jambo Festival , Afisa Masoko wa Jambo Food Products Company  ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo, Anthony Paul amesema kwa mwaka huu zawadi zimeongezeka hadi kufikia milioni 22.

Naye Mratibu wa mashindano hayo Zena Mchujuko alisema maandalizi yanaenda vizuri hivyo wananchi wote ndani ya Mkoa wa Simiyu na nje ya Mkoa wajitokeze kwa wingi kushiriki mashindano hayo.

Simiyu Jambo Festival mwaka  2018 inadhaminiwa na Jambo Food Products Company, UNFPA, Maswa Standard Chalks, Meatu Milk, NGS Petroleum Limited, Alliance Ginneries Ltd, NGM Gold Mine Limited, SIBUKA na Busega  Mazao Limited.

MWISHO

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa