• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Naibu Spika awataka Watanzania Kutobeza Ngoma za Asili na Michezo

Posted on: July 8th, 2018

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson ametoa wito kwa wananchi kutobeza ngoma za asili na michezo na badala yake waone fursa zilizopo katika Michezo na Utamaduni ili ziweze kuwanufaisha.

Dkt. Tulia ameyasema hayo Julai 08, wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Simiyu katika  Tamasha la SIMIYU JAMBO FESTIVAL Mjini Bariadi, ambalo limehusisha mashindano ya ngoma za asili (Wagika na Wagalu), mbio za baiskeli(Kilomita 150 wanaume na kilomita 100 wanawake), mbio fupi(Kilomita 10 na Kilomita tano), uandishi wa insha, likiwa limeshirikisha washiriki kutoka  mikoa mbalimbali hapa nchini, nchi jirani ya Kenya.

Amesema wapo watu wengi amabao wamepata fursa ya kusafiri kwenda maeneo mbalimbali hapa dunia na kujipatia fedha kutokana na ngoma asili zinazotambulisha utamaduni wa makabila yao pamoja na michezo mbalimbali hivyo maeneo hayo hayatakiwi kubezwa.

“Niwaombe ndugu zangu isitokee mtu yeyote akafikiri ngoma za asili au michezo ni vitu vya kubeza, haya ni mambo ambayo kama nchi tumekuwa nayo na tunataka kuendelea nayo, wapo watu wametembea nchi nyingi duniani kwa sababu ya ngoma za asili na michezo, tuendelee kuunga mkono juhudi zinazofanywa kuendeleza michezo na utamaduni” alisema.

Akizungumzia kauli mbiu ya SIMIYU JAMBO FESTIVAL mwaka 2018 inayosema Familia Yangu, Furaha Fangu, Afya Yangu amepongeza ubunifu wa mkoa wa Simiyu kuja na kauli mbiu hiyo ambayo inatoa hamasa kwa wananchi kuona umuhimu wa kuthamini afya zao na akalishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) kwa kuboresha miundombinu ya Afya katika Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa  wa Simiyu utabaki kuwa kielelezo katika Utamaduni huku akibainisha kuwa wamedhamiria kuufanya (kuuza) utamaduni wa mkoa huo ambao watu hucheza ngoma za asili na wanyama kama nyoka na fisi ili wananchi waweze kuona kunufaika na utamaduni wao.

Mhe. Mtaka amewashukuru wadhamini wa SIMIYU JAMBO FESTIVAL mwaka 2018  kwa namna walivyofanikisha, ambapo amesema mwaka huu wigo wa tamasha hilo umepanuliwa kwa kuongeza mashindano ya mbio fupi, uandishi wa insha tofauti na mwaka 2017 ambapo kulikuwa na mashindano ya mbio za baiskeli na ngoma za asili(Wagika na Wagalu)  

Ameongeza kuwa amesema matarajio yake ni kuona mkoa wa Simiyu na Tanzania kwa ujumla inatoa wachezaji wa mchezo wa Mbio za baiskeli katika mashindano ya Olimpiki mwaka 2020, kupitia mashindano ya michezo mbalimbali iayofanyika katika Simiyu Festival.

Naye Mdhamini Mkuu wa Simiyu Jambo Festival mwaka 2018 Mhe. Salum Khamis mmiliki wa Jambo Food Products amesema kampuni yake itaendelea kudhamini tamasha hilo ambapo ameahidi kuwa mwaka 2019 itaongeza zawadi kutoka milioni 25 mwaka 2018 na kufikia milioni 35.

Kwa upande wao wananchi wa mkoa wa Simiyu wamesema Tamasha la Simiyu Jambo Festival mwaka 2018 limefana, limechangia kwa kiasi kikubwa kuutangaza Mkoa wa Simiyu hasa kupitia utamaduni wa Wagika na Wagalu na mchezo wa baiskeli na kusaidia kuchangia uchumi wa watu wa Simiyu.

“Yaani leo mji wa Bariadi wote umesimama kwa sababu ya tukio hili ambalo kwa mwaka huu limekuwa kubwa zaidi ya mwaka jana, halafu hata wafanyabishara wa Bariadi wamenufaikakupitia tukio hili, tumuombe Mkuu wetu wa mkoa aendelee kutuletea mambo yenye manufaa kwa wananchi wake.

Tamasha la Simiyu Jambo Festival mwaka 2018 lilishirikisha washiriki kutoka mikoa 13 hapa nchini na nchi jirani ya Kenya huku likihusisha mashindano ya mbio za baiskeli (kilomita 150 wanaume, kilomita 100 wanawake, kilomita 10 walemavu), mashindano ya mbio fupi(kilomita 10 na kilomita tano), mashindano ya ngoma za asili(Wagika na Wagalu) na mashindano ya uandishi wa insha kwa wanafunzi wa shule za sekondari.

Katika mashindano ya Mbio za Baiskeli wanaume kiliometa  150 Richard Laizer kutoka Arusha cha alishika nafasi ya kwanza na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 1.2 aliyekimbia Kilometa 150 na kwa uapnde wa wanawake  Laulensia Ruzuba kutoka Mwanza aliyekimbia km 100 kwa dakika 3:06:20 aliibuka mshindi wa kwanza na kujipatia shilingi 1,000,000/=

Mkoa wa Simiyu pia ulifanya vizuri ambapo mchezaji wake Elizabeth Mwinamila ambaye alikimbia Km 100 kwa saa 3:10:58 alipata kiasi cha Sh. 800,000 akifuatiwa na Sophia Adson kutoka Arusha ambaye alikimbia kwa saa 3:15:47.

Kwa upande wa mbio fupi kilometa 10 Mshindi wa kwanza wanawake Esther Chesenga na wanaume Joseph Mbatha kutoka nchini Kenya walijinyakulia kitita cha shilingi 1,000,00/= na nafasi ya pili kwa wanaume ilichukuliwa na Fabian Sulle huku wanawake ikichukuliwa na Failuna Matanga

Simiyu Jambo Festival imefanyika kwa mara ya pili sasa mkoani Simiyu na litakuwa likifanyika kila mwaka likiwa ujumbe tofauti wa kufikisha kwa jamii.

 

Wanautamaduni wakionesha umahiri wao wa kucheza na nyyoka wakati wa Tamasha la SIMIYU JAMBO FESTIVAL Mjini Bariadi, ambalo limehusisha mashindano ya ngoma za asili (Wagika na Wagalu), mbio za baiskeli(Kilomita 150 wanaume na kilomita 100 wanawake), mbio fupi(Kilomita 10 na Kilometa tano), uandishi wa insha, likiwa limeshirikisha washiriki kutoka  mikoa mbalimbali hapa nchini, nchi jirani ya Kenya.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa