Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa, Dkt. Edmund B. Mndolwa amewaongoza viongozi wa CCM Taifa na Mkoa wa Simiyu, viongozi wa Serikali Mkoa wa Simiyu na wananchi wa Wilaya za Meatu na Maswa katika mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Kata ya Tindabuligi Marehemu Mahega Selemani Kijiji cha Zebeya wilayani Maswa, ambaye alifariki dunia Juni 10 katika ajali iliyotokea kwenye msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James katika Kijiji cha Kisesa wilayani Meatu.
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Dkt. Mndolwa ametoa pole kwa familia ya marehemu Mahega na akawaomba ndugu na familia kuwa na subira katika kipindi kigumu walichonacho.
Amesema Mhe. Rais anatoa shukrani kwa Kituo cha Afya Mwandoya, Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu, Hospitali ya Rufaa Bugando na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa namna walivyowahudumia majeruhi 19 wa ajali hiyo ambapo baadhi yao walitibiwa na kuruhusiwa na wengine bado wanaendelea kupata matibabu.
Aidha, Dkt. Mdolwa amemshukuru Mbunge wa Kisesa ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina kwa kuchukua maamuzi ya haraka ya kukodi ndege iliyowapeleka majeruhi tisa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James ametoa pole kwa familia, ndugu, wananchi wa Tindabuligi na kuwashukuru viongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa msaada walioutoa toka siku ile ajali ilipotokea katika kuhakikisha wanasaidia kunusuru maisha ya wote waliojeruhiwa katika ajali ile.
"Ninawashukuru sana viongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa namna walivyolishughulikia suala hili, kila niliyempigia simu baada ya ajali juhudi zake zilionekana; kwa kweli Simiyu mmedhihirisha ukamilifu wa mapenzi, ushirikiano na moyo wa kusaidia wengine"'alisema Kheri James.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa pole kwa familia, ndugu na Baraza la Madiwani Meatu amewashukuru viongozi wa Chama na Serikali ambao wametoa misaada mbalimbali katika kuhakikisha majeruhi wa ajali wanapata matibabu kwa wakati na marehemu anasitiriwa kwa heshima zote kama kiongozi.
Katika hatua nyingine Mtaka amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kuhakikisha kuwa stahili zote za kisheria ambazo familia ya marehemu inapaswa kupewa na Halmashauri, zitolewe mapema badala ya kusubiri kufuatwa na familia hiyo.
Naye Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa iliko kata aliyokuwa anaitumikia marehemu Mahega amewashukuru viongozi wa Chama na Serikali kwa namna walivyojitoa katika kushughulikia majeruhi na msiba ambapo pia amewashukuru wananchi wa Wilaya ya Meatu na Maswa mahali alikozikwa marehemu kwa ushirikiano na upendo mkubwa waliounesha katika msiba huo tangu siku Mhe. Mahega alipofariki mpaka kuzikwa kwake.
Mpina ametoa pole kwa familia, wananchi wa kata ya Tindabuligu na Wilaya ya Meatu kwa ujumla kwa kuondokewa na Mhe. Mahega ambaye amesema ameacha pengo kubwa kwa kuwa alikuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya wananchi na Meatu kwa ujumla.
Kwa upande wake Diwani wa Viti maalum Mhe. Avelina Kyakwambala ambaye amefanya kazi na Marehemu kama madiwani toka mwaka 2000 , amesema msiba huo umeupokea kwa masikitiko makubwa na kwamba Meatu imepoteza diwani mwadilifu, mchapakazi, anayezingatia kanuni zote za baraza, chama chake na alikuwa tayari kukosoa na kukosolewa kwa ajili ya kujenga na kuleta maendeleo kwa wananchi.
Msiba wa Marehemu Mahega Selemani ambaye ameacha mke na watoto 14, umehudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Viongozi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Simiyu na Mwanza na Viongozi wa Serikali Mkoa wa Simiyu na wilaya zote mkoani humo.
MWISHO
Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mahega Selemani aliyekuwa Diwani wa Kata ya Tindabuligi Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, ambaye alifariki kwa ajali kwenye Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James Juni 10, 2018 katika Kijiji cha Kisesa wilayani Meatu , likiwekwa kaburini tayari kwa mazishi ambayo yamefanyika Kjiji cha Zebeya Wilayani Maswa.
Kutoka kulia Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani, Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Benson Kilangi wakiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Mahega Selemani aliyekuwa Diwani wa Kata ya Tindabuligi katika Halmashauri hiyo mkoani Simiyu, ambaye alifariki kwa ajali kwenye Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James Juni 10, 2018 katika Kijiji cha Kisesa wilayani Meatu , wakati wa mazishi yaliyofanyika Kjiji cha Zebeya Wilayani Maswa.
Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Bw. Erasto Sima na Mbunge wa Jimbo la Meatu, Salum Khamis wakiteta jambo katika Msiba wa Marehemu Mahega Selemani aliyekuwa Diwani wa Kata ya Tindabuligi Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, ambaye alifariki kwa ajali kwenye Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James Juni 10, 2018.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Mahega Selemani aliyekuwa Diwani wa Kata ya Tindabuligi Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, ambaye alifariki kwa ajali kwenye Msafara wake akiwa ziarani Mkoani humo, Juni 10, 2018 katika Kijiji cha Kisesa wilayani Meatu , wakati wa mazishi yaliyofanyika Kjiji cha Zebeya Wilayani Maswa.
Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Bw. Erasto Sima wakiteta jambo katika Msiba wa Marehemu Mahega Selemani aliyekuwa Diwani wa Kata ya Tindabuligi Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, ambaye alifariki kwa ajali kwenye Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James Juni 10, 2018 katika Kijiji cha Kisesa wilayani Meatu , wakati wa mazishi yaliyofanyika Kjiji cha Zebeya Wilayani Maswa.
Mjane wa marehemu Mahega Selemani aliyekuwa Diwani wa Kata ya Tindabuligi Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, ambaye alifariki kwa ajali kwenye Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James Juni 10, 2018 katika Kijiji cha Kisesa wilayani Meatu, akiweka shada la maua kwenye kaburi la mume wake wakati wa mazishi yaliyofanyika Kjiji cha Zebeya Wilayani Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Mahega Selemani aliyekuwa Diwani wa Kata ya Tindabuligi Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, ambaye alifariki kwa ajali kwenye Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James Juni 10, 2018 katika Kijiji cha Kisesa wilayani Meatu , wakati wa mazishi yaliyofanyika Kjiji cha Zebeya Wilayani Maswa.
Baadhi ya waombolezaji katika Msiba wa Marehemu Mahega Selemani aliyekuwa Diwani wa Kata ya Tindabuligi Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, ambaye alifariki kwa ajali kwenye Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James Juni 10, 2018, katika Kijiji cha Kisesa wilayani Meatu kabla ya mazishi yaliyofanyika Kjiji cha Zebeya Wilayani Maswa
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Khadija Shaban maarufu kama Keisha akizungumza na waombolezaji katika Msiba wa Marehemu Mahega Selemani aliyekuwa Diwani wa Kata ya Tindabuligi Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, ambaye alifariki kwa ajali kwenye Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James Juni 10, 2018 katika Kijiji cha Kisesa wilayani Meatu, kabla ya mazishi yaliyofanyika Kjiji cha Zebeya Wilayani Maswa.
Mbunge wa Viti maalum( CCM) Mkoa wa Simiyu akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Mahega Selemani aliyekuwa Diwani wa Kata ya Tindabuligi Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, ambaye alifariki kwa ajali kwenye Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James Juni 10, 2018 katika Kijiji cha Kisesa wilayani Meatu , wakati wa mazishi yaliyofanyika Kjiji cha Zebeya Wilayani Maswa.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa