• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Mwenge wa Uhuru Kupitia Miradi ya Bilioni 8 Mkoani Simiyu

Posted on: July 4th, 2017

MWENGE wa Uhuru umeanza mbio zake rasmi leo katika mkoa wa Simiyu ambapo utapitia jumla ya miradi 43 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 8,450,841,622/=.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati akitoa salamu za Mkoa huo kwa Kiongozi wa kitaifa wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 , Ndg.Amour Hamad Amour katika kijiji cha Bukundi wilaya ya Meatu ukitokea katika mkoa Singida.

Mtaka amesema kati ya fedha hizo shilingi 680,285,524 zinatokana na Nguvu za wananchi ,Serikali Kuu shilingi 4,524,439,388, Halmashauri Shilingi 352,000,875,
Washirika wa Maendeleo Shilingi 635,559,935 na Sekta binafsi Shilingi 2,258,555,900/=

Amesema Mwenge wa Uhuru utafungua miradi 14, kuzindua 13, kutembelea na kuona miradi 16 katika sekta ya Elimu,Afya,Maji,Vijana na wanawake, Miundombinu ya barabara, Sekta ya Viwanda, Maliasili, Kilimo, Ushirikana Utawala bora.

Aidha, Mtaka amesema katika kutekeleza kwa vitendo ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wa mwaka huu 2017 usemao “SHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YANCHI YETU”, Mkoa wa Simiyu umeweza kujipambanua katika utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda kupitia Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja, Bidhaa Moja, Kiwanda Kimoja”


“Katika utekelezaji huu mkoa umefanikiwa kuanzisha kiwanda cha Chaki wilayani Maswa, Kiwanda cha Maziwa wilayani Meatu na Upembuzi yakinifu unaendelea mingine minne ambayo pia itatekelezwa katika Halmashauri zetu nyingine nne”  amesema Mtaka.

Ameongeza katika miradi kuwa kukamilika kwa viwanda hivyo kutasaidia kutoa ajira kwa vijana wa mkoa wa Simiyu na mikoa jirani kutokana na kuwa malighafi zinazotumika na zitakazotumika katika viwanda hivyo zinazalishwa hapa nchini.

Naye kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru , Ndg. Amour Hamad Amour akifungua jengo la upasuaji kwa wanawake wajawazito katika kituo cha Afya Bukundi wilayani Meatu mbali na kuipongeza wilaya hiyo kwa kujali afya za wananchi wake hususani wanawake wajawazito pia alitaka mradi huo utunzwe na uthaminiwe.

“Mradi huu ni mzuri na mimi nimefurahi kuona naanza kuzindua miongoni mwa miradi inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja, hasa akinamama wajawazito hivyo basi nitoe wito kwa wanawake kutumia vizuri jengo hili badala ya kujifungulia majumbani hali inayoweza kuhatarisha afya zenu, vile vile mradi huu utunzwe na kuthaminiwa ili uendelee kutusaidia,”alisema.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa wilaya ya Meatu wameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza miradi ambayo imewasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali katika huduma za jamii ikiwemo maji na afya kwa kuwa itawasaidia kupata huduma hizo karibu na kwa ubora unaotakiwa.

“Wakina mama wengi walikuwa wanapoteza maisha kwa kujifungulia njiani , kwa kweli naishukuru sana serikali maana kuwepo kwa jengo la upasuaji lililozinduliwa leo na mwenge wa uhuru,kutatusaidia sana ” amesema Tatu Athumani mkazi wa Bukundi.



Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa