• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Mwenge wa Uhuru Kupitia Miradi 36 Simiyu Yenye Thamani Ya Zaidi ya Shilingi Bilioni Nane

Posted on: August 14th, 2018

Jumla ya miradi 36 yenye thamani ya shilingi  bilioni 8.4  iliyopo katika Halmashauri sita za Mkoa wa Simiyu itapitiwa na Mwenge wa Uhuru ambao umeanza rasmi mbio zake mkoani humo, Agosti 15, 2018.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akisoma salamu za mkoa wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha bukundi wilayani Meatu ukitokea wilaya ya Mkalama Mkoani Singida Agosti 14, 2018.

Mtaka amesema kuwa miradi hiyo inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru ni kutoka katika Idara ya Elimu, Afya, Maji, Viwanda, Kilimo, Maliasili, Barabara,Utawala, Sekta binafsi na Vijana na Wanawake.

Akizungumzia Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 ambao umejikita zaidi katika Elimu kwa kauli Mbiu “ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA; WEKEZA SASA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU” amesema, Elimu ni kipaumbele cha kwanza kwa mkoa huo, ambapo wameweka mikakati mbalimbali ya kuinua elimu na ujenzi wa miundombinu ya elimu.

 

“ Simiyu ni mkoa pekee ambao wanafunzi wa madarasa ya mitihani wanakaa katika kambi za kitaaluma, pia ufaulu wa wanafunzi wetu umeongezeka mfano, mwaka 2017 mkoa wa Simiyu ulikuwa wa 26 Kitaifa kati ya mikoa 31 lakini mwaka 2018 mkoa umeshika nafasi ya 10 katika matokeo ya kidato cha Sita” alisema.

Aidha, Mtaka amesema Simiyu inaendelea kuboresha miundombinu ya elimu kwa kushirikisha jamii na wadau mbalimbali ikiwa na mkakati wa kujenga shule tatu ambazo ni Shule ya Sekondari ya Ufundi Simiyu, Shule ya Sekondari ya Wasichana na Shule ya Sekondari ya Wavulana.

Hata hivyo Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Meatu umepita katika miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa vyumba vya madarasa katika shule shikizi ya Mwanyahina, Mradi wenye majengo manne katika Hospitali ya Wilaya; (jengo la wodi ya wazazi, jengo la upasuaji, maabara na nyumba ya mtumishi), mradi wa ujenzi wa mahakama ya mwanzo Itinje na mradi wa ushonaji wa wanawake wa Kijiji cha Mwamishali.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho amewataka viongozi na watendaji kusimamia miradi ya maendeleo kwa weledi na kuhakikisha inatekelezwa kwa wakati kwa  viwango vinavyohitajika na kuzingatia thamani ya fedha(value for maoney) ili wananchi wapate huduma.

“Utawala wa Awamu ya tano unataka watu wafanye kazi na kuwajibika kweli,tunaposema HAPA KAZI TU Mhe. Rais anamaanisha, tukisimamia miradi kwa ulegelege hatutaweza kufika, inawezekana hata kuchelewa kwa miradi ni kwa sababu watu wanataka maslahi yao na kusababisha huduma za kijamii zinakwama ili wao wanufaike, watendaji wa aina hiyo awamu ya tano hatuwahitaji” alisema Kabeho

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani akizungumza mara baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kuweka jiwe la msingi mradi wa madarasa ya shule shikizi ya Mwanyahina amesema Viongozi wa wilaya watasimamia ujenzi wa mradi huo na kuhakikisha unajengwa  kwa viwango na kwa wakati ili shule hiyo iwanufaishe wananchi wa vijiji jirani vinavyoizunguka.

Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake mkoani Simiyu katika Wilaya ya Meatu Agosti 14, 2018, Agosti 15 utakuwa halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Agosti 16 Halmashauri ya mji wa Bariadi, Agosti 17 Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Agosti 18 Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Agosti 19 Halmashauri ya Wilaya ya Maswa na tarehe Agosti 20, utakabidhiwa mkoani Shinyanga.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGIO HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/08/mwenge-wa-uhuru-kupitia-miradi-36.html

 

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa