• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Mwekezaji Kutoka Malaysia Anatarajia Kuwekeza Mradi wa Dola Bilioni 2.5 Pori La Akiba la Kijereshi Simiyu

Posted on: November 23rd, 2019

Mwekezaji Azhar Malik kutoka Nchini Malaysia ameonesha nia ya kuwekeza kiasi cha Dola za kimarekani bilioni 2.5 katika mradi mkubwa eneo la pori la akiba la Kijereshi na Ziwa Victoria wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, sehemu ya uwekezaji huo ikiwa ni katika ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji, utamaduni na maeneo mengine yatakayoimarisha utalii na kutoa ajira kwa wananchi.

Mwekezaji ambaye amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Dkt. Ramadhan Dau amesema ikiwa kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa ikiwemo mradi huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwezi Januari 2020, huku akisisitiza kuwa utatekelezwa bila kuathiri ikolojia na mazingira ya uhifadhi.

“Nashukuru kwa ushirikiano nilioupata kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, pia namshukuru Balozi Dau kwa namna alivyolisimamia jambo hili tangu likiwa wazo mpaka sasa tunapoelekea kwenye utekelezaji niwaahidi tu kuwa pale pande zote zitakapofanya maamuzi mikataba ikisainiwa kwa mujibu wa sheria, mwakani mwezi Januari tutaanza utekelezaji,”alisema Malik

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Dkt. Ramadhan Dau amepongeza uongozi wa Chama na Serikali kwa utayari walioonesha, akisisitiza ushirikiano wa viongozi hao na taasisi zote za Serikali zinazohusika, ili mambo yote muhimu yanayohitajika kufanikisha uwekezaji huo yafanyike mapema  kuanzia mwezi Januari kazi ianze.

“Kwa kasi na namna tulivyoanza lile lengo tulilojiwekea kwamba ikifika Januari 2020 mambo yote yanayohusiana na taratibu na  kusaini mikataba, yanapaswa yawe yamekamilika na wataalam waje site (eneo la mradi) waanze survey (utafiti) watengeneze master plan(mpango kabambe), ili kabla ya mwezi Juni 2020 hili jambo liwe limeanza,” alisema Balozi Dau.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema Uwekezaji huu utaupambanua Mkoa wa Simiyu, Kanda ya Ziwa na kuupambanua utalii kwenye uso wa dunia, ambapo amebainisha kuwa mradi huu utajibu mahitaji mengi kwenye ajira na kukua kwa maendeleo ya ukanda huo.

Kwa upande wao Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) wameahidi kutoa ushirikiano ili kuhakikisha mradi huu unafanikiwa.

Mradi huu wa uwekezaji katika sekta ya utalii wilayani Busega utatekelezwa kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza inatarajiwa kugharimu takribani dola bilioni 500 na mpaka kukamilika kwake utagharimu dola za Kimarekani bilioni 2.5.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/11/mwekezaji-kutoka-malaysia-anatarajia.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa