• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Mwekezaji Kutoka India Aonesha Nia Kuwekeza Kilimo cha Mpunga, Kiwanda cha Kuchakata Mpunga Simiyu

Posted on: January 9th, 2020

Mwekezaji kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala ameonesha nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kupitia umwagiliaji na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega mkoani Simiyu, ambapo anatarajia kuwekeza katika eneo lenye ukubwa wa ekari zipatazo 2000.

Akizungumza na viongozi na watendaji wa Mkoa wa Simiyu baada ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye fursa ya uwekezaji katika kilimo cha mpunga wilayani Busega, Bw. Agarwala amesema mkoa wa Simiyu na Tanzania kwa ujumla ina rasilimali nyingi hivyo ikiwa Makampuni kutoka India yatafanya kazi kwa kushirikiana na Watanzania rasilimali hizo ziatakuwa na manufaa kwa Watanzania.

“Mkoa wa Simiyu na Tanzania kwa ujumla ina rasilimali za kutosha ambazo zipo kwa ajili ya kuwanufaisha Watanzania wenyewe hivyo  kinachohitajika ni teknolojia, uwekezaji, ushirikiano kutoka Serikalini kufanya haya yote yatokee; baada ya ziara hii ninaamini tukiyatekeleza kwa juhudi yale tuliyokubaliana mkoa huu utaendelea kwa kasi,” alisema Agarwala.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemhakikishia mwekezaji huyo upatikanaji wa eneo la ekari 2000 kwa ajili ya uwekezaji na kubainisha kuwa malengo ya mkoa ni kuhakikisha wilaya ya Busega inakuwa mzalishaji mkuu wa chakula katika mkoa kwa kuwa ndiyo wilaya yenye ziwa Victoria ndani ya Mkoa.

Aidha, pamoja na kutoa ushirikiano kwa mwekezaji kutimiza azma yake Mtaka amesema Serikali ya Mkoa imezungumza na Benki ya CRDB kuona uwezekano wa kuwawezesha wakulima wa mpunga wilayani Busega hususani walio kando ya ziwa Victoria kupitia dirisha la kilimo ili waweze kulima kisasa kupitia umwagiliaji.

Naye Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Bw. Lusingi Sitta amesema Benki iko tayari kumuunga mkono mwekezaji na wakulima wa wilaya ya Busega  kupitia dirisha la kilimo kutokana na wilaya hiyo kuwa na maeneo mazuri na chanzo cha uhakika cha maji (Ziwa Victoria), ambapo alibainisha kuwa tayari benki hiyo ina uzoefu wa kuwezesha miradi mbalimbali ya kilimo cha umwagiliaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo amesema wao kama chama wanaunga mkono juhudi za watu wanaoitika huku akiongeza kuwa mkoa huo ni miongoni mwa mikoa inayofanya vizuri kwenye kilimo hususani cha mpunga hivyo ujio wa mwekezaji huyo mkoani hapa utasaidia kuongeza tija kwenye zao hilo.

Katika hatua nyingine baadhi ya wakulima wamesema kuwa ujio wa mwekezaji huyo utawasaidia wao kuzalisha kwa tija ikilinganishwa na awali," tukianza kulima kilimo cha umwagiliaji tunaamini tutavuna mavuno mengi maana tutalima zaidi ya mara moja kwa msimu" alisema Monika Msabila

"Kuna kipindi mavuno yanashuka kama mvua zikiwa chache sasa ujio wa mwekezaji huyu tumeupokea maana atatusaidia na sisi kulima kilimo cha umwagiliaji na kuacha kutegemea mvua pekee " alisema Simon Ngelela mkazi wa Kijiji cha Shigala wilayani Busega.

Katika hatua nyingine mwekezajI alipata fursa ya kutembelea kiwanda kinachomilikiwa na Mwekezaji mzawa, Deogratius Kumalija ambacho kinaongeza thamani kwenye mazao ya chakula hususani mpunga na mahindi Busega Mazao Limited  kilichopo wilayani Busega.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/01/mwekezaji-kutoka-india-aonesha-nia.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa