• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Mwalimu Aliyetoa Alama A 90 Mtihani wa Taifa Darasa la Saba Apewa Tuzo Mkoani Simiyu

Posted on: May 2nd, 2018

Mwalimu Akwilina Ernest Marenge kutoka Shule ya Msingi Salunda katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, amepata zawadi ya shilingi 500,000/= kwa ajili ya pongezi kwa kufanikiwa kutoa Alama A kwa wanafunzi 90 kati ya wanafunzi 147 katika Somo la Kiswahili katika mtihani wa Darasa la Saba mwaka 2017.

Fedha hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka kwa mwalimu huyo mbele ya baadhi ya viongozi wa mkoa huo, wanafunzi na walimu wengine wa Shule ya Msingi Salunda.

Akikabidhi fedha hizo Mtaka amesema Serikali imetambua juhudi za mwalimu huyo ambaye Katika somo lake la Kiswahili alikuwa na ufaulu mzuri ambapo alitoa alama A 90, Alama B 55 na Alama C 2, hivyo kama kiongozi ameona ni vema mwalimu huyu akapewa motisha.

"Siku ya Mei Mosi alipewa shilingi laki tano kama mfanyakazi hodari na mimi nikasema nitampa shilingi 500,000 za kwangu siyo za Serikali, kama kiongozi niliona ni jambo la kupongezwa, Fedha hii haifanani na alichofanya kwa watoto ila najua wanafunzi wake watamkumbuka daima" alisema Mtaka.

Kwa upande wake Mwl. Akwilina Marenge ambaye anatarajia kustaafu mwezi Juni mwaka 2018 amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka kwa kutambua juhudi zake na kuona umuhimu wa kumpongeza na akatoa wito kwa walimu wengine kujituma na kupenda kazi yao.

Nao Walimu wenzake na Mwalimu Akwilina wamempongeza na kubainisha kuwa anastahili kupata zawadi zote hizo kwa kuwa pamoja na kuwa umri mkubwa amekuwa ni mtu wa kujituma na kufanya kazi kwa bidii zaidi ya walimu vijana.

"Mwalimu Akwilina ni mwalimu wa tofauti na walimu wengine, pamoja na kwamba yeye umri wake umekwenda sana anawahi kazini, anaipenda kazi yake, anajituma kuliko hata walimu vijana, ni mcheshi; hata sasa hivi tunavyosikia anaenda kustaafu tunasikitika kwa sababu anaondoka mtu mchapakazi" alisema mwalimu Tabitha Erasto.

" Huyu mama ni mtu mzima lakini anajituma kuliko baadhi ya walimu vijana ni kitu cha kushangaza mno, japo anaelekea kustaafu sisi wenzake tunaobaki tunapaswa tuige mfano wake kwa kweli" Alisema Mwalimu Joyce Mishana.

Akitoa shukrani kwa niaba ya walimu wengine Mwalimu Mkuu wa Shule ya Salunda, Mwl. Nchambi Tupendane amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa kutambua mchango wa mwalimu Akwilina na kubainisha kuwa zawadi hiyo imekuwa ni chachu kwao ya kufanya vizuri zaidi katika Mtihani wa Taifa mwaka huu na miaka ijayo.

Kutokana na utendaji kazi mzuri Mwalimu Akwilina pia alitambuliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kuwa Mfanyakazi Hodari na siku ya Mei Mosi alizawadiwa shilingi laki tano na cheti

MWISHO 

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU MAKABIDHIANO HAYO FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/05/mwalimu-aliyetoa-alama-90-mtihani-wa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa