Na Stella Kalinga
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa ushirikiano uliopo kati ya Ofisi yake,Wakuu wa Wilaya ,Wakurugenzi wa Halmashauri, utaufanya mkoa huo kuwa balozi mzuri kwa wananchi kujiunga kwenye mfuko Taifa wa Bima ya Afya.
Mtaka ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Bima ya afya (NHIF) uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katolini na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko huyo Taifa Anne Makinda, ambao ulikuwa na lengo kubaini changamoto zinazowakabili wanachama wa Mfuko huo sambamba na utoaji wa elimu juu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya. Amesema kuwa wananchi kujiunga na mfuko huo ni muhimu sana kwani watapunguza gharama kubwa wakati wa matibabu na wanapaswa kutambua kuwa ugonjwa huingia mwilini bila taarifa.
“..Ushirikiano tutakaoonesha sisi viongozi juu ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya utawasaidia wananchi kuokoa gharama kubwa ya fedha wakati wa kupata matibabu…na kujiunga uanachama ndio njia pekee rahisi na kisasa katika kupata matibabu duniani kote…Alisema
Aidha Katika kufikia dhamira ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ya Tanzania ya viwanda na kuwa na nguvu kazi iliyo salama kiafya, ameiomba Bodi ya Mfuko huo wa Bima ya afya kuanzisha ofisi za Mkoa, ili kuwarahisishia wananchi wa mkoa huo upatikanaji wa huduma.
Awali akitoa taarifa ya Maboresho ya huduma kwa wanachama na wadau wa mfuko wa Bima ya afya Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya afya Taifa Leonard Konga alieleza kuwa Mfuko huo umeanzishwa kwa dhamira ya kutoa Bima ya afya kwa makundi mbalimbali ya wananchi, Kujenga uwezo wa kifedha kwa vituo na kushirikisha sekta binafsi katika kuharakisha maendeleo ya sekta ya afya.
Konga alitaja mafanikio ya utekelezaji wa shughuli za Bima ya afya yanategemea kila mdau kutimiza wajibu wake kwani mazingira ya kiutendaji ni kusimamia na kutekeleza miongozo na maagizo ya serikali kupitia wizara yenye dhamana ya kusimamia upatikanaji wa huduma za afya. Alibainisha kuwa lengo mahususi katika utekelezaji wa mpango wa Mfuko wa Bima ya afya kuw ni pamoja na kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma za afya kuanzia ngazi ya Zahanati hadi ngazi ya hospitali ya Mkoa na Kuongeza wigo mpana zaidi kwa watanzania wanaopata huduma za matibabu kupitia Bima ya Afya. Naye Kaimu Meneja wa wa Bima ya afya Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya Mkoa wa Shinyanga Immanuel Imani alizitaja changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na Upungufu wa dawa katika baadhi ya vituo, Ukosefu wa vifaa tiba na ubovu wa majengo, waajiri kuchelewesha madai pamoja na uchache wa watoa huduma.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya afya Taifa (NHIF) amesema kuwa katika maeneo mengi aliyopita amebaini kuwa wananchi wengi wanatumia fedha zao kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya lakini wanapoenda kuhudumiwa wanakumbana na matusi pasipo kupata huduma bora.
Amesema kuwa Bodi yake imekusudia kuboresha huduma za matibabu kwa wananchi sambamba na kupinga vikali lugha chafu zitolewazo na baadhi ya watoa huduma katika sekta ya afya dhidi ya wananchi wanaoenda kupata matibabu katika Zahanati, Vituo vya afya, Hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa