Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas amekutana na viongozi wa Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi,Oktoba 02, 2018 kwa lengo la kujadiliana namna ya kutangaza utekelezaji wa shughuli za Serikali.
Mkutano huo ulihusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi na Wakuu wa Idara wa Halmashauri na Mkoa.
Katika mkutano huo, Dkt. Abbas aliwasisitiza viongozi hao umuhimu wa kutekeleza, kutangaza na kutetea shughuli na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali..
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas(kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) na Katibu Tawala Mkoa, Bw. Jumanne Sagini mara baada ya Mkutano wake na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiongozwa na Mhe. Anthony Mtaka (katikati) am Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas ambao ulifanyika Oktoba 02, 2018.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa