Bohari ya Dawa (MSD) inatarajia kujenga kiwanda cha kutengeneza bidhaa za afya zitokanazo na pamba hususani gozi na bandeji katika Mkoa wa Simiyu.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD , Brigedia Jenerali Dkt. Gabriel Mhidze wakati wa ziara yake aliyoifanya Juni 24, 2020 mkoani Simiyu kwa lengo kukutana na viongozi wa mkoa, kuangalia eneo la ujenzi wa kiwanda hicho na kutembelea moja ya viwanda vya kuchambua pamba wilayani Bariadi.
“Kama MSD tutatengeneza gozi, bandeji zile ndogo za vidonda na hata zile pamba za masikioni lakini tutaanza kwa awamu kwanza, lakini naamini bidhaa nyingine za pamba pia tutazitengeneza,” alisema Dkt. Mhidze.
Aidha, Dkt. Mhidze amesema kwa sasa bidhaa hizo zinaagizwa kutoka nje ya nchi hivyo ikiwa zitaanza kuzalishwa hapa nchini kutakuwa na soko la uhakika la bidhaa hizo (vifaa tiba).
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema viongozi wote watatoa ushirikiano wote unaotakiwa na MSD huku akimhakikishia Mkurugenzi Mkuu wa MSD upatikanaji wa nguvu kazi kwa kiwanda hicho.
Kwa upande wake Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo kata ya Kasoli wilayani Bariadi, Bw. Boaz Ogolla amemhakikishia Mkurugenzi Mkuu wa MSD upatikanaji wa malighafi ambayo ni pamba hai kutoka kwa wachambuzi wa pamba (ginners ) wa ndani ya nchi na hususani Mkoa wa Simiyu.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/06/msd-yajipanga-kujenga-kiwanda-cha.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa