Mrembo Diana Anthony kutoka wilaya ya Meatu jana ameibuka mshindi wa kwanza kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Simiyu mwaka 2019 lilioshirikisha jumla ya warembo 15 hivyo kupeperusha bendera ya ulimbwende mkoa wa Simiyu na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja.
Shindano la kumtafuta mlimbwende yamefanyika Julai 6, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, huku Mgeni rasmi akiwa naibu spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson yakisindikizwa na burudani ya kutoka kwa mwanamuziki anayetamba ndani na nje ya nchi Nasibu Abdul almaarufu Diamond Platnumz
Shindano hili limeamuliwa na Majaji wanne ambapo mionggoni mwao wamewahi kuwa Miss Tanzania katika nyakati mbaimbali Saida Kessy (1997), Hoyce Temu aliyeshinda taji la miss Tanzania mwaka 1999, mtaalamu wa kuibua vipaji nchini Rita Paulsen maarufu madam Rita na Anitha Kagemulo.
Washindi wengine wanne wa shindano la Miss Simiyu 2019 wanaotengeneza tano bora ni Rebeca Manoti, Miriam Palangyo, Neema Ismail na Angel Mathew.
Akizungumza kabla ya kuwatangaza washindi watano wa Shindano la Miss Simiyu 2019, Jaji Mkuu wa Shindano hilo, Hoyce Temu (Miss Tanzania 1999) alisema warembo walioshiriki katika shindano hilo wanavigezo vyote vya kufikia Miss Tanzania.
“Kwa mara ya kwanza Simiyu imefanya maajabu sijawahi kuona warembo wa namna hii na kama hawatafika Miss Tanzania hawa basi mimi nidaiwe na majaji wenzangu” alisema Hoyce Temu.
Akikabidhi zawadi ya Miss Simiyu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson aliwataka washiriki wote wa Taji la Miss Simiyu kufanya mambo mazuri ili wawe mfano mzuri wa kuigwa.
Aidha kampuni ya halotel Tanzania pia ilitoa zawadi kwa ya simu za mkononi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tano .
Wadhamini wa mashindano hayo yaliyoandaliwa na Simiyu Talent Company kwa kushirikiana na Grace Entertainmen .ni Jambo Food products Company, Friedkin Conservation Fund, Busega Mazao, Halotel Tanzania na Diamond rock.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:https://simiyuregion.blogspot.com/2019/07/mrembo-dayana-anthony-atangazwa-miss.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa