• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Mrajisi Atakiwa Kutoa Vibali kwa Wafanyabiashara Kusafirisha Choroko

Posted on: March 1st, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amemuagiza Mrajisi msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Simiyu, Bw. Ibrahim Kadudu kutoa vibali kwa wafanyabiashara wa choroko kwa ajili ya kusafirisha maeneo mbalimbali mara bada ya kulipa ushuru wa Halmashauri na Vyama vya msingi vya Ushirika (AMCOS).

Agizo hilo lilitolewa jana na kuwasilishwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi.Miriam Mmbaga wakati wa kuhitimisha kikao cha mkoa cha wadau wa zao la choroko kilichofanyika Machi 01, 2021 Mjini Bariadi kwa ajili ya kujadili utaratibu wa uuzaji choroko.

“Mrajisi unatakiwa utoe vibali vya kusafirisha choroko ambazo zipo tayari, na vibali hivyo vitolewe mara baada ya wafanyabiashara hao kulipa ushuru wa Halmashauri na AMCOS; ili kuepusha usumbufu ni vema tukaweka utaratibu ili kuhakikisha kuwa malipo yote yanafanyika Halmashauri,”

“Ili Mkulima na mfanyabishara waweze kunufaika na bidhaa za kilimo ni vyema kila mmoja wao akafuata taratibu, Kanuni na sheria zilizotolewa na Tume ya Ushirika, kwa msimu huu wa choroko ni vyema Choroko zote ziingie kwenye minada, hii Itamsaidia mkulima kupata bei shindani,” alisema.

Awali akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alitoa wito kwa viongozi kulijadili suala la ununuzi wa Choroko na kufanya maamuzi kulingana na mazingira ya mkoa ili kulinda maslahi ya Serikali, Mkulima na Mfanyabiashara.

Aidha, Mtaka ameongeza kuwa badala ya wakulima kuwekewa vikwazo, ni vema ikaangaliwa namna ya kuwasaidia wakulima kwa kuwa zao la choroko  limekuwa zao la pili la biashara, Mkoani Simiyu baada ya zao la pamba.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitia mkoa wa Simiyu, Mhe. Gungu Silanga akichangia hoja katika kikao hicho ameshauri kuwa wakulima na wafanyabiashara wapewe elimu zaidi kuhusu mfumo wa stakabadhi ghalani waelewe ili utumike wakati mwingine lakini kwa sasa wakulima wapewe uhuru wa kuuza choroko zao kupitia mfumo huo au soko huria.

Aidha, amewasisitiza Wafanyabiashara kuhakikisha  wanalipa ushuru na tozo zote wanazopaswa kulipakama inavyoelekezwa na Serikali.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa Wa Simiyu, Bw. John Sabu amesema ni vema Vyama vya Ushirika  vitafute mtaji navyo viingie sokoni kununua choroko kama wafanyabiashara wengine na ili kumuepushia usumbufu Mfanyabiashara ni vyema Malipo yote ya ushuru yafanyike mahala pamoja.

Mbunge wa Kisesa, Mhe.Luhaga Mpina amesema Mwongozo wa stakabadhi ghalani umekuja wakati wakulima tayari wameshalima yaani baada ya biashara na tayari wafanyabiashara wameshaingia gharama hivyo  lipewe muda na wakulima/ wafanya biashara waelimishwe.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bariadi, Mhe. Juliana Mahongo amependekeza kuwa Ushirika uangaliwe kwa nchi nzima,na upelekwe msaada bungeni ili kuhakikisha kwamba ushirika wetu unaimarishwa kwa manufaa ya wananchi na si kuwakandamiza watu.

Mrajisi Mkoa wa Simiyu Bw. Ibrahim Kadudu amesema Ilani ya Chama kuhusu ushirika ni kusogeza huduma kwa wananchi na kuboresha maisha ya wananchi na kusisitiza kuwa Mfumo wa stakabadhi ghalani ulianza mwaka 2020, na wakulima walikubali kwamba wataanza kutumia mfumo huo mwaka huu.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2021/03/mrajisi-atakiwa-kutoa-vibali-kwa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa