• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Mrajis Awataka Maafisa Ushirika Kuimarisha Usimamizi wa Vyama vya Ushirika

Posted on: June 9th, 2020

Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege amewataka Maafisa Ushirika kuimarisha usimamizi katika vyama vya ushirika ili kuhakikisha vyama hivyo vinatekeleza majukumu yake kwa uadilifu na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za ushirika.

Dkt. Ndiege ametoa agizo hilo wakati akizungumza na maafisa ushirika wa mkoa wa Simiyu katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani Simiyu Juni 09, 2020.

 

“Wekeni mpango wa kuvitembelea vyama vya ushirika ili kuona shughuli zinazofanyika na kuweka usimamizi imara ili kuondoa dhana ya kufanya uchunguzi, ni bora kugundua tatizo kabla halijatokea na kulidhibiti kuliko kusubiri litokee na kuanza kuchukua hatua,” alisema Dkt. Ndiege.

 

Aidha, Dkt. Ndiege amewasisitiza Maafisa ushirika kufuatilia makusanyo ya mfuko wa usimamizi na ukaguzi kutoka Vyama vya Ushirika ili kupata fedha za kusimamia Vyama hivyo, huku akiwahakikishia kuwa fedha zote za makusanyo zitaendelea kuletwa kwao ili waongeze usimamizi na kuimarisha Ushirika.

Wakati huo huo Dkt. Ndiege ameitaka  Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu (SIMCU) kuhakikisha inaweka mipango madhubuti ya utoaji huduma kwa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) na kuvisimamia kwa ukaribu zaidi na kuhakikisha vinatekeleza majukumu inavyopaswa.

Katika hatua nyingine Dkt.Ndiege ametoa wito kwa Bodi ya chama Kikuu cha ushirika mkoa wa Simiyu (SIMCU) na Chama Kikuu cha Ushirika Shinyanga (SHIRECU)  kufanya maridhiano juu ya mgawanyo wa mali ili kuendeleza uwekezaji katika mali hizo, ikiwemo viwanda vya kuchambua pamba vya Luguru, Sola na Malampaka vilivyopo Simiyu.

Mwenyekiti wa Bodi wa SIMCU Bw. Emanuel Mwerere amesema kuwa makubaliano ya mgawanyo wa mali yamechelewa kutokana na  wanachama wa SIMCU kupitia Mkutano Mkuu kukubali kupokea mali pekee kutoka SHIRECU na hawakuwa tayari  kupokea madeni, huku akibainisha kuwa hawakuchukua viwanda hivyo kwa ajili ya kukwepa hasara katika uendeshaji kutokana na hali ya viwanda hivyo ilivyo kwa sasa ambayo hairidhishi.

Kwa upande wake Mrajisi Msaidizi wa Mkoa Bw. Ibrahim Kadudu kupitia taarifa ya Ushirika ya Mkoa amesema Vyama vya Ushirika vya pamba Mkoani humo vinakabiliwa na changamoto ya malipo ya ushuru kiasi cha shilingi bilioni 3.9 na bado wakulima zaidi ya 11,047 wanadai fedha zao za pamba kiasi cha shilingi bilioni 3.4.

Naye Meneja wa Bariadi Teachers SACCOS Bw. Nchimbi Yahya akiwasilisha taarifa kwa Mrajis ameomba  fedha za akiba za wanachama wao zinazoshikiliwa na Wakurugenzi wa Halmashauri ziweze kurejeshwa, ambapo Mrajis amekiri kulifahamu suala hilo na kuahidi kulitafutia ufumbuzi.

MWISHO

 KUPATA PICHA ZAIDI TAFADHALI FUNGUA KIUNGANISHI (LINKI) HIKI HAPA CHINI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/06/mrajis-awataka-maafisa-ushirika.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa