Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Venance Mabeyo ametembelea wilaya ya Itilima na Bariadi.
Akiwa Wilaya ya Itilima Jenerali Mabeyo alikabidhi madarasa 2,Ofisi Moja na vyoo matundu nane, yaliyojengwa na Meja Jenerali Paulo Kisesa kwa ushirikiano na Wanajeshi wenzake.Akiwa kwenye hafla hiyo aliahidi kutoa kiasi cha Tsh. 30m ambazo zitatumika kukamilisha baadhi ya Miundo mbinu ambayo ni Ofisi ya waalimu.
Aidha Jenerali ameahidi akiwa Wilaya ya Bariadi Kata ya Matongo, Kijiji cha Matongo, aliahidi kuchangia kiasi Tsh.50m ili kukamilisha ujenzi wa shule ya wasichana Matongo-Bariadi ambayo majengo yake yaliachwa tangu mwaka 2010 wakati Simiyu ikiwa sehemu ya Shinyanga.Mwisho.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa