• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Mhe.Kafulila Azindua Bodi Ya Parole Mkoani Simiyu

Posted on: March 4th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila hivi karibuni amezindua Bodi ya Parole, Mkoani Simiyu. Akizungumza na wajumbe wa Bodi  wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo, Mhe. Kafulila amesema “ninyi mkiwa wajumbe wa Bodi mna wajibu wa kuamua kwa haki stahili za wafungwa. Cha kukumbuka siku zote ni kuwa, Rais wetu  Mama Samia Suluhu Hassan, suala la haki lipo kwenye moyo wake,mbali ya sheria ya nchi pamoja na katiba, suala la haki lipo kwenye moyo wa Mhe Rais. Hivyo nanyi  mkiwa wasaidizi wake mnapaswa kuhakisi hiyo haki. Mpaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Hamad Masauni anawateua ninyi, mchakato mkubwa umepita,hivyo bila shaka mnauwezo na uzoefu mkubwa,nanyi pia ni wenye haki’’.Pitieni  vizuri sheria zote zinazohusiana na kazi yenu ili mjue sheria na taratibu zinasema nini, ili mnapofanya maamuzi yawe maamuzi ya haki yanayozingatia, sheria, taratibu na kanuni.

Akizungumza Kamishna Msaidizi wa Magereza Mkoa wa Simiyu ACP. Huruma.E Mwalyaje,ameeleza kuwa kuzinduliwa kwa Bodi ya Parole Mkoa wa Simiyu, ni mafanikio makubwa sana kwa mkoa, kwani hii ni bodi ya kwanza kuzinduliwa na kufanya kikao chake cha kwanza mkoani Simyu.Kabla ya hapo Mkoa wa Simiyu haukuwa na Bodi yake ya Parole na hivyo kupelekea shughuli zote na maamuzi yotye yanayohusu Magereza mkoa wa Simiyu,kufanywa na  Bodi ya Parole ya  Mkoa wa Shinyanga.

ACP. Mwalyaje ameeleza kuwa Bodi hiyo ina wajumbe watano, ambapo kati yao wajumbe wanne ni wanaume na mmoja wa kike. Majina ya wajumbe hao ni Zongo Said ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi, Sheikh Mahmoud Salum kalokola - mjumbe, Dkt.Phillips Mtiba-mjumbe,Bi.Margareth Magele-mjumbe na Mchungaji Marco Fabian Mringo- mjumbe.

Akizungumza mwenyekiti wa Bodi ya Parole Simiyu Bw. Zongo Said amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwazindulia Bodi na kwa ushauri aliowapatia wa kusimamia haki nao wameahidi kuwa watazingatia hilo. Bw.Said amewataka wale wanaoanzisha masuala ya haki na stahili za wafungwa wawe makini na watende kwa haki ili wao kama watekelezaji,wasipotoshwe na hivyo kufanya maamuzi yanayozingatia haki, taratibu na sheria.Mwisho.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa