• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Meatu yatakiwa Kubuni Vyanzo Vipya vya Mapato, Kuongeza Vituo vya Biashara

Posted on: July 2nd, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuongeza vituo vingine vya biashara  ili iweze kuongeza hali ya ukusanyaji wa mapato.

Mkuu wa Mkoa huyo aliyasema hayo jana wakati akizungumza na madiwani na watendaji wa Halamshauri hiyo kwenye kikao cha Baraza maalumu la madiwani llililokuwa na agenda moja ya kujadili hoja 21 za ukaguzi zilizoibuliwa na mkaguzi na mthibiti mkuu wa hesabu za serikali(CAG).

“ Anzisheni vyanzo vipya vya mapato lakini pia fungueni miji mipya ya kibiashara mfano kule Bukundi daraja limeshajengwa hatuwezi kujenga daraja la Sabaiti halafu kukaendelea kuwa pori, ni lazima Bukundi uwe mji mwingine wa kibiashara kama Mwandoya, Mwanhuzi na ‘centres’ nyingine na karibisheni sekta binafsi” alisema.

Katika hatua nyingine amewakaribisha wafanyabiashara wa mabasi kupeleka magari yao Meatu ili kuwarahisishia wananchi huduma za usafiri kwenda Makao makuu ya mkoa na kuondoa changamoto ya usafiri iliyopo ambapo ni kampuni moja tu inayofanya kazi wilayani humo na akawaasa polisi kutojihusisha na uonevu dhidi ya wafanyabiashara na wananchi.

Kuhusu hoja za ukaguzi zilizoibuliwa na wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Meatu kujibu hoja za ukaguzi zilizoibuliwa na mkaguzi na mthibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG)kuhakikisha zinajibiwa kwa wakati na kwa ufasaha huku akiwataka wataalam kutoa ushirikiano kwa mkaguzi wa ndani.

Mtaka pia amemtaka mkaguzi wa ndani wa Halmashauri hiyo kuwa jicho ili aisaidie halmashauri hiyo wakati wakitekeleza miradi mbalimbali huku akisisitiza hoja zijibiwe kwa wakati bila ubabaishaji zikienda sambamba na viambatanisho vya vielelezo vinavyojitosheleza.

Fabian Manoza ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na mkuu wa mkoa huo na kuhalikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa mkaguzi wa ndani .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Pius Machungwa alisema kwa mwaka 2016/2017 mkaguzi na mthibiti Mkuu  10 wa hesabu za serikali aliibua hoja za ukaguzi 91 ambapo walipata hati ya mashaka, hivyo kwa mwaka huu wametekeleza baadhi ya mapendekezo na kuwafanya kupata hati safi.

Alisema kwa mwaka huu (2017/18) mkaguzi ameibua hoja za ukaguzi 24 na kuifanya halmashauri hiyo kupata hati safi huku akiahidi kusimamia miradi ili waendelee kupata hati safi na pia kumtumia mkaguzi wa ndani katika usimamizi wa miradi

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Fabian Manoza alisema hoja nyingi zilitokana na mambo ya ndani ambayo watendaji walitakiwa kuyadhibiti hasa yatokanayo na ukusanyaji wa mapato ambapo wameanza kukusanya mapato kwa mfumo wa kielektroniki (EFD).

Manoza alisema watamtumia mkaguzi wa ndani wanapotekeleza miradi ili endapo akibaini kuna mapungufu aweze kuwajulisha na wayafanyie kazi.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/07/meatu-yatakiwa-kubuni-vyanzo-vipya-vya.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa