• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Mavunde Awataka Viongozi Kuwatumia Watoa Msaada wa Kisheria Kutatua Matatizo ya Wananchi

Posted on: October 21st, 2019

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde amezindua rasmi Maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria ambayo yanafanyika Kitaifa

Mkoani Simiyu na kutoa wito kwa viongozi wa Serikali kuwatumia wasajili wasaidizi na watoa huduma za kisheria kutatua matatizo ya kisheria yanayowakabili wananchi.

Akizungumza na wananchi Oktoba 21, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi  Mkoani Simyu Mavunde amesema matatizo ya kisheria yanashughulikiwa kisheria na siyo kisiasa hivyo ni vema wakawashirikisha na wakaambatana nao hata katika ziara zao ili waweze kutoa msaada wa kisheria kila unapohitajika.

“Yapo mambo mengi sana ambayo ni ya kisheria wananchi mmekuwa mkikimbilia kwa viongozi wa kisiasa, siasa ina sehemu yake inakoma inabaki sheria, wiki ya msaada wa kisheria ni fursa ya kipekee kuelewa namna ya kushughulikia matatizo yenu na mnaendelea kujifunza kuwa sheria inabaki kuwa sheria na utatuzi wake unakuwa katika mfumo uliowekwa kisheria,” alisema Mavunde.

Awali akitoa taarifa ya wiki ya msaada wa kisheria  Msajii wa Taasisi za watoa huduma za kisheria, B. Felistas Mushi amesema lengo la kuwepo wa huduma ya msaada wa kisheria ni kuhakikisha haki inapatikana kwa wananchi wasioweza kumudu gharama za wawakili”tunaamini kuwa baada ya maadhimisho haya kutakuwa na mtazamo chanya katika kutatua matatizo ya wananchi kisheria.”

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka ametoa wito kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu wahakikishe katika ziara zao wanaambatana na wasajili wasaidizi na watoa huduma za kisheria walio katika maeneo yao ili waweze kutatua na kutoa ushauri wa namna ya kutatua matatizo yote kisheria.

Aidha, amewataka viongozi na wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya vijiji, kata na wilaya kuhakikisha kuwa wanatumia vizuri mafunzo wanayopewa na wakayatafsiri kwa vitendo katika utatuzi wa matatizo ya watu kwa haki na kushirikiana na viongozi wa Serikali, taasisi na vyombo vyote vya maamuzi.

Katika hatua nyingine Mtaka ameshauri kuwa ingekuwa vema pia kama masuala ya kisheria yakajumuishwa katika baadhi ya masomo kama vile somo la Uraia ili kuendelea kujenga uelewa wa pamoja juu ya namna ya kukabiliana na matatizo yote ya kisheria.

Kwa upande wake Mkuugenzi Mtendaji wa TANLAP, Bi. Christina Ruhinda ameiomba Serikali na taasisi zake kushirikiana na watoa huduma za kisheria ili huduma hizo ziwe endelevu na matatizo ya wananchi yaweze kufanyiwa kazi kwa haki.

Mkurugenzi wa Miradi Shirika la Legal Services Facility, Bi. Scholastica Jullu amesema shirika ilo litaendelea kufadhili mashirika yanayotoa msaada wa kisheria kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa kisheria mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu “Msaada wa Kisheria kwa Maendeleo Endelevu”, wakati yakiadhimishwa kitaifa mkoani SIMIYU yanapotarajiwa kuhitimishwa Oktoba 25, 2019 pia yanaadhimishwa katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro,Mbeya, Mtwara, Mwanza, Njombe, Ruvuma, Shinyanga, Tabora na Tanga.

MWISHO

KUPATA PICHA ZADI FUNGUAA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/10/naibu-waziri-mavunde-awataka-viongozi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa