Naibu Waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana na ajira Mhe. Anthony Mavunde ameziagiza halmashauri zote nchini kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali kwa vijana na wanawake..
Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo Agosti 02, 2020 ambayo imetengwa maalum kwa ajili ya kuhamasisha Programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP)baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020, katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.
“Mhe. Waziri Mkuu wa awamu ya tatu alitoa maelekezo ya kutenga maeneo hayo, awamu ya nne akaja Mzee Pinda Novemba 2014 likaja azimio la kila mkoa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali kwa vijana na wanawake, mpaka sasa zimetengwa hekari 203,000 tu ambazo bado hazitoshi kulingana na ukubwa wa nchi yetu, kwa hiyo kuna baadhi ya mikoa ambayo haijatekeleza ” alisema Mavunde
Mhe. Mavunde amesema Ofisi ya Waziri Mkuu inashirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI vijana wanawezeshwa kushiriki katika Kilimo kupitia mradi wa Vitalu nyumba ambapo vijana 100 kwa kila halmashauri wamepewa mafunzo na mpaka sasa vijana takribani 18,000 wamefikiwa lengo likiwa ni kuwafikia vijana huku lengo likiwa ni kuwafikia vijana 45,000 kwa awamu ya kwanza.
Ameongeza kuwa kwa sasa vijana wamehamasika sana kufanya shughuli za kilimo tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma ambapo kilimo kinafanywa na watu waliokosa kazi nyingine, hivyo akaendelea kusisitiza maeneo maaluma kwa ajili ya shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwemo kilimo na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao.
Katika hatua nyingine Mavunde ametoa kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi kujifunza teknolojia mbalimbali zitakazoongeza tija na thamani katika kazi wanazofanya ikiwemo kilimo, mifugo na uvuvi.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amesema mkoa huo uko tayari kitoa maeneo kwa ajili ya shughuli za uzalishaji ikiwemo kilimo huku akiahidi kuendelea kushirikiana na Wizara ya Kilimo kuhakikisha Programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP) haibaki katika maandishi bali inaingia katika vitendo.
Naye Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema utekelezaji wa Programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP) unahitaji fedha hivyo akatoa rai kwa taasisi za fedha kuongeza fedha katika sektaya kilimo, mfugo na uvuvi ambazo zinagusa sehemu kubwa ya maisha ya watu, ambapo amesisitiza wizara ya kilimo, ofisi ya Waziri Mkuu na wizara ya fedha kulifanyia kazi hilo.
Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2020 ni ya tatu sasa katika Mkoa wa Simiyu ambapo Kauli Mbiu ya maonesho hayo mwaka huu ni “KWA MAENDELEO YA KILIMO , MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020.”
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-http://simiyuregion.blogspot.com/2020/08/mavunde-aagiza-halmashauri-kutenga.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa