Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga ameutaka uongozi wa Wilaya ya Maswa kumsimamia Mkandarasi SUMA JKT anayejenga kiwanda cha chaki na kiwanda cha vifungashio wilayani humo ili akamilishe ujenzi wa viwanda hivyo kwa wakati ili vianze uzalishaji.
Nyamhanga ameyasema hayo wakati wa ziara yake alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa viwanda hivyo eneo la Ng’hami ambapo ameutaka uongozi wa Wilaya ya Maswa kufuatilia uagizaji wa mitambo ya kiwanda cha chaki huku akiahidi kuwa ofisi yake itafuatilia kibali cha kuagiza Mitambo kwa ajili ya kiwanda cha vifungashio. katika Ofisi ya HAZINA(Wizara ya Fedha)ili miradi yote iende sambamba.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa