• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kufunguliwa rasmi kesho Oktoba 16 Simiyu

Posted on: October 15th, 2019

Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  yanatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho  Oktoba 16, 2019 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Mjini Bariadi Mkoani hapa, ambapo washiriki kutoka taasisi za Umma na binafsi zaidi ya 100, mifuko ya uwezeshaji zaidi ya 40 na vikundi vya kijamii (VICOBA) wanatarajiwa kushiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 15, 2019 Mjini Bariadi Afisa Uhusiano Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), Bw. Edward Kessy  ambao ndiyo waandaaji amesema maonesho haya ni fursa kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa kujifunza huduma za mifuko ya uwezeshaji, taasisi za fedha na programu mbalimbali.

“Maonesho haya yameanza Oktoba 14, 2019 na yatafunguliwa rasmi Oktoba 16, 2019 na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na yatahitimishwa tarehe 20 Oktoba, 2019 na Mhe. Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, nitoe wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili waje wajionee huduma mbalimbali za mifuko, taasisi na vikundi vya kijamii,” alisema Kessy.

Afisa Biashara wa Taasisi ya Private Agricultural Sector Support (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine Mungo ametoa wito kwa wananchi kutembelea banda lao kujua huduma zao, huku akibainisha kuwa Taasisi hiyo kupitia mpango mkakati wa miaka mitano ulioanza mwaka 2018 inatarajia kuzifikia familia 235,000 kwa kudhamini mikopo kiasi cha shilingi bilioni 210.6 .

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Posta Tanzania tawi la Bariadi, Bw. Shadrack Daudi amesema benki hiyo kwa kushirikiana na NEEC na PASS imetoa mikopo ya vikundi mbalimbali vya kijamii, vikundi rasmi na visivyo rasmi, wafanyabiashara, hivyo ni vema wananchi wafike kwa wingi kujionea fursa hizo ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Naye mnufaika wa mikopo ya mifuko ya uwezeshaji, Bw. Emmanuel Nyambi Katibu wa Chama cha Ushirika cha Msingi kutoka Kahama, ametoa wito kwa wananchi kufika katika maonesho hayo ili waweze kuona fursa za upatikanaji wa mikopo kupitia mifuko, programu na taasisi mbalimbali za kifedha huku akieleza kuwa hakuna urasimu katika utoaji wa mikopo.

“Natoa wito kwa wajasiriamali wadogo au vyama mbalimbali, wafike kwenye maonesho haya waje wajifunze namna ya kupata mikopo ya kuendeshea shughuli za kiuchumi, niwahakikishie hakuna urasimu kwenye mikopo, tunaipata kwa wakati na Benki Kuu inadhamini kikubwa ni kuwa waaminifu kurejesha mikopo,” alisema Nyambi.

Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu: “Mitaji ni Chachu ya Kujenga Tanzania ya Viwanda”.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII TAFADHALI TEMBELEA BLOGU YETU YA MKOA KUPITIA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/10/maonesho-ya-mifuko-ya-uwezeshaji.html

 

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa