• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Madeni ya Pamba Kulipwa Kabla ya Msimu Mpya: Katibu Mkuu Kilimo

Posted on: April 30th, 2020

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Kusaya amesema Serikali itahakikisha madeni yote ya Vyama vya Msingi vya ushirika(AMCOS), wakulima, ushuru wa Halmashauri  na Vyama Vikuu vya Ushirika kwa zao la pamba ambayo bado hayajalipwa yanalipwa kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa mwaka 2020.

Kusaya ameyasema hayo Aprili 29, 2020 katika kikao alichofanya na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na wanunuzi wa pamba ambacho kimefanyika Mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara ya siku moja mkoani Simiyu.

“Serikali inayatambua madeni yote kwenye zao la pamba AMCOS na Vyama Vikuu vya Ushirika vinadai, Halmashauri zetu nazo zinadai ushuru lakini pia hata kwenye mfuko wa pembejeo; ni lengo la serikali na jitihada zinazofanywa na wizara ya Kilimo na wizara nyingine kwa kuwa hili ni suala mtambuka, kuhakikisha madeni yote yanamalizika kabla hatujaanza msimu mpya ,” alisema Kusaya.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Vyama vya msingi havijalipwa, wakulima 7000 hawajalipwa na Halmashauri, hazijalipwa ushuru wa pamba takribanishilingi bilioni 3.5,  ambapo amebainisha kuwa mapato ya ndani ya Halmashauri yanategemea ushuru wa pamba kwa asilimia 70 hivyo madeni hayo yameathiri shughuli za uendeshaji wa Halmashauri.

“ Wakulima wetu 7000 bado wanadai fadha za kilo milioni 2.6, AMCOS zinadai shilingi bilioni 3.5, Chama chetu Kikuu cha Ushirika kinadai milioni 729, Halmashauri zetu zinadai bilioni 3.5 ni vema jambo hili likafanyiwa kazi na  (maeneo hayo) viungo vyote hivi kwenye zao la pamba vikaunganishwa vizuri ili kuwe na ufanisi katika msimu ujao,” alisema Mtaka.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa Pamba nchini, Bwana Boazi Ogolla akitoa taarifa kwa niaba ya wanunuzi amesema wanunuzi wanaiomba Serikali kutekeleza ahadi yake ya kulipa fidia ya hasara waliyopata wanunuzi mara baada ya kununua pamba kwa bei elekezi ya shilingi 1200 ambayo ilikuwa juu zaidi ya bei ya soko la dunia.

Ogolla amesema kushindwa kulipwa fidia hiyo kumesababisha wanunuzi kushindwa kulipa ushuru wa pamba kwa Halmashauri, vyama vya ushirika, madeni ya wakulima, malipo ya mchango wa mfuko wa pembejeo, madeni ya watoa huduma na benki(wakopeshaji).

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo ameitaka serikali kutimiza ahadi hiyo ya kuhakikisha madeni yote yanalipwa kabla ya msimu kuanza ili msimu mpya usiwe na vikwazo vyovyote.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Musabila Kusaya amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Kilimo linalojengwa viwanja vya Nane nane Nyakabindi Bariadi, Simiyu na kumtaka mkandarasi ambaye ni Suma JKT kuhakikisha ujenzi unakamilika kabla ya Mei 30, 2020.


Ujenzi wa jengo hilo ulianza mwaka jana 2019 na lilitakiwa kukamilika machi 30 na hadi sasa limefikia asilimia 70 ya ujenzi huku changamoto ikitajwa kuwa ni mabadiliko ya mchoro.

MWISHO

 KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/04/madeni-ya-pamba-kulipwa-kabla-ya-msimu.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa