Mwandishi wa Vitabu Bw. Richard Mabala ametoa msaada wa nakala 120 za vitabu vya fasihi vya "Hawa The Bus Driver" na "Mabala the Farmer " kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili katika shule za Mkoa wa Simiyu.
Akikabidhi msaada huo Novemba 06, 2020 kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime amewataka wanafunzi hao kujisomea vitabu hivyo wapate maarifa yatakayowasaidia katika mitihani yao na maisha kwa ujumla ili kutimiza kusudi la mtoa msaada huo.
“Mvitumie vitabu hivi vizuri, mkijenga tabia ya kujisomea kuanzia kidato cha kwanza na cha pili mtakapofika kidato cha tatu na cha nne fasihi kwenu itakuwa rahisi kwenu; hakikisheni mnautumia msaada huu vizuri msome na siku moja akija Simiyu tutamleta awaulize maswali,” alisema Simime.
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa Shule, Mkuu wa Shule ya Sekondari Bariadi, Mwl. Ally Simba amemshukuru Mwandishi wa Vitabu Ndg. Richard Mabala ambapo amesema wameupokea msaada huo kwa mikono miwili huku akimhakikishia kuwa vitabu hivyo vitasomwa na wanafunzi na vitasaidia kuongeza ufaulu katika mitihani yao.
Nao wanafunzi wa Shule ya sekondari Bariadi wakizungumza kwa niaba ya wanafunzi wao wa mkoa wa Simiyu wameshukuru kupata msaada huo na kuahidi kuutumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Tunamshukuru sana Mabala kwa msaada wake na tumeupokea kwa mikono miwilitunaahidi tutasoma kwa bidii vitabu hivyo na vitatusadia kujibu maswali ipasavyo ili tuweze kufaulu katika mitihani yetu,” alisema Kija Nyerere mwanafunzi wa kidato cha Kwanza Bariadi sekondari.
“Msaada huu una faida sana kwetu maana vitabu vinaelimisha, vinaburudisha naamini tutafanya vizuri katika mitihani yetu kwa sababu pia itatusaidia kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuachana na mila potofu,” alisema mwakilishi wa wanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Bariadi.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/11/blog-post.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa