Naibu waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba ametembelea Viwanja vya Nyakabindi kujionea maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakatofanyika kuanzia Julai 28, 2019 hadi Agosti 08, 2019 katika Viwanja Vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu, ambapo ameridhishwa na maaandalizi hayo ambayo amesema kwa sasa yamefikia zaidi ya asilimia 75.
Amesema maandalizi ya mwaka huu ni tofauti na mwaka jana kutokana na mwaka jana kwa sababu mwaka jana yalikuwa ya dharura lakini mwaka huu taasisi zimejipanga na baadhi ya zimeanza kujenga majengo ya kudumu katika Viwanja vya Maonesho.
“ Maandalizi ya mwaka huu ni tofauti na mwaka jana kwa sababu mwaka jana yalikuwa ni ya dharura lakini kwa udharura ule ule tulifanikiwa kufanya vizuri lakini mwaka huu, maandalizi yamekuwa tofauti kwa sababu majengo ya kudumu yameongezeka na niwahakikishie watu wote watakaokuja kwenye maonesho mwaka huu kupata vitu vizuri” alisema Mgumba.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wadua wengine kushiriki katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 huku akiwahakikishia kuwa maonesho hayo yatakuwa makubwa sana hivyo wategemee matokeo makubwa pia.
Kwa upande wake Mratibu wa Nanenane kutoka Wizara ya Kilimo, Dkt. Kissa Kajigili amesema barabara zinazozunguka uwanja zenye urefu wa kilometa sita zimeshachongwa na visima vinne vya maji vinachimbwa kuongeza idadi ya viwili vilivyopo ili kuboresha huduma ya maji katika viwanja vya Nyakabindi.
Ameongeza kuwa Halmashauri zote 21 za Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga inayounda Kanda ya Nanenane ya Ziwa Mashariki na taasisi nyingine zimepanda vipando vya mazao mbalimbali kwa ajili ya kuwaelimisha wakaulima, wafugaji na wavuvi ambavyo vinaendelea vizuri.
Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yataanza tarehe 28 Julai, 2018 na yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan Agosti 01, 2019 na kufungwa Agosti 08, 2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/07/maandalizi-ya-maonesho-ya-nanenane.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa