Maafisa elimu na wakuu wa shule zote za sekondari Mkoani Simiyu wametakiwa kuhakikisha wanasimamia ukamilishaji wa ujenzi wa maboma ya vyumba vya madarasa kabla ya kufikia Aprili 20,mwaka huu ili kuruhusu wanafunzi waliokosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwaka 2019 waweze kuanza masomo.
Wito huo umetolewa Machi 13, 2019 na Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.Ernest Hinju wakati wa kikao cha kuweka mikakati madhubuti ya elimu Mkoani humo.
Hinju amesema kuwa maafisa elimu wote pamoja na wakuu wa shule za sekondari wanatakiwa kusimamia vema ujenzi wa maboma hayo ili yaweze kukamilika kwa wakati wakati na ubora unaotakiwa.
Ameongeza kuwa ni lazima ukamilishaji huo ,ukawa ndani ya muda uliokusudiwa kwani tayari Serikali imeshaziwezesha shule kiasi cha shilingi 12,500,000/= (kwa chumba kimoja) kwa ajili ya ukamilishaji wa majengo hayo kwa haraka.
Naye Edda Malick kiongozi wa Mpango wa kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP T) amesema kwa upande wao wameweza kukamilisha ujenzi wa maboma kwa asilimia 60.
Malick ameongeza kuwa wameweza kufikia asilimia hizo kutokana na jitihada na usimamizi madhubuti wa maafisa elimu na wakuu wa shule
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/03/maafisa-elimu-wapewa-siku-37.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa