• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Kuelekea Mtihani wa Taifa 2019, RC Mtaka Awafunda Darasa la Saba Simiyu

Posted on: September 9th, 2019

Kuelekea katika Mtihani wa Taifa wa Kuhitimu elimu ya Msingi Darasa la saba Septemba 11-12, 2019 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewaonya wanafunzi wa darasa la saba mkoani hapa kujiepusha na udanganyifu katika mtihani huo badala yake wazingatie yale waliyofundishwa na kufanya mtihani huo kwa utulivu na kujiamini.

Mtaka ameyasema hayo Septemba 09, 2019 wakati akizungumza na wanafunzi wa darasa la saba kutoka katika Kata ya Lamadi wilayani Busega Septemba 09, 2019 katika Shule ya Msingi Mwabasabi, kwa niaba ya wenzao wa Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kuwatakia heri katika  mtihani wa Taifa wanaotarajia kuufanya kuanzia Septemba 11-12, 2019.

Mtaka amesema anaamini walimu wamefanya kazi yao vizuri ya kuwafundisha na kuwaandaa wanafunzi  hao hivyo ni vema wakafanya mtihani huo wakiwa na ujasiri huku wakipuuza taarifa zozote za kuwepo kwa majibu ya mitihani mahali popote.

“Ninawatakia kila la heri kwenye mtihani wenu, nashukuru kwa kazi nzuri iliyofanywa na walimu katika kuwafundisha na kuwaandaa kwa kutoa majaribio ya mara kwa mara, kambi kambi za kitaaluma; niwaombe mkaufanye mtihani huu kwa utulivu na ujasiri; asiwadanganye mtu kuwa kuna majibu ya mtihani au mtihani umevuja sehemu fuulani, mkazingatie mlichofundishwa” alisema Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka amewashukuru walimu kwa namna wanavyojituma katika kuwafundisha wanafunzi na kutoa wito kwa walimu hao kuanzisha madarasa ya maandalizi ya kidato cha kwanza (pre- form one)  kwa wanafunzi hao wanaohitimu ili wasaidie kuwaandaa wanafunzi hao na  masomo ya kidato cha kwanza na waweze kupata kipato cha ziada kupitia malipo yatakayotolewa na wazazi watakaokuwa tayari kugharamia masomo hayo.

Kwa upande wake Afisa Taaluma Mkoa wa Simiyu , Mwl. Onesmo Simime amesema Mkoa wa Simiyu uliweka mikakati mbalimbali ya maandalizi ya wanafunzi wa darasa la saba ikiwemo walimu kumaliza mada zote mwezi Juni 2019 na kuwepo kwa kambi za kitaaluma kwa kila shule,  hivyo wanafunzi wameandaliwa vizuri na kwa mikakati hiyo matarajio ya mkoa ni ufaulu kuongezeka zaidi ya mwaka jana 2018.

Akizungumza kwa niaba ya walimu, Mwalimu Beatrice Ernest kutoka Shule ya Msingi Mwabasabi amesema wana uhakika na maandalizi waliyofanya kwa wanafunzi wao hivyo  ufaulu utaongezeka, huku akimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwaruhusu kuanzisha vituo vya ‘pre-form one’ na kuahidi kuwa walimu watajiunga kuanzisha madarasa hayo ili kuboresha taaluma ya wanafunzi wao na kuboresha vipato vyao.

Nao baadhi ya wanafunzi wakizungumza kwa niaba ya wenzao wamesema wamejiandaa vizuri na wamejipanga  kufanya vizuri ili waweze kutimiza malengo yao ikiwa ni pamoja na  kujiunga na elimu ya sekondari na hatimaye kuendelea na elimu juu ili waweze kufikia ndoto zao.

“Mimi na wenzangu wote tumejiandaa vizuri nina uhakika tutafanya vizuri na wote tutaenda sekondari, ushauri tuliopewa na Mkuu wa Mkoa tutauzingatia naamini tutashinda tu” Eric Malimi kutoka Shule ya Msingi Lamadi.

“Sisi tumejiandaa vizuri na tunaweza kuendelea mbali kimasomo, tunamshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kutupa mawaidha na tutayatekeleza ili tuweze kufaulu mtihani wa Taifa na tufikie tunapotaka” alisema  Glorymary Samwel kutoka Shule ya Msingi Itongo.

Mkoa wa Simiyu una jumla ya wanafunzi 29,248  wa darasa la saba wanaotarajia kufanya mtihani wa Taifa Septemba 11-12, mwaka huu, ambao kati yao  wavulana ni  13, 594 na wasichana 15.654.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/09/kuelekea-mtihani-wa-taifa-2019-rc-mtaka.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa