• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Kituo cha Afya Lukungu Chatakiwa Kuimarisha Mfumo wa Ukusanyaji, Usimamizi Mapato

Posted on: September 10th, 2020

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba ameutaka uongozi wa Kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega kuimarisha ukusanyaji na usimamizi wa mapato (kudhibiti upotevu wa mapato) ili kuongeza mapato yatakayosaidia kununua dawa na kuboresha miundombinu kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Dkt. Kulemba ameyasema hayo Septemba 10, 2020 katika nyakati tofauti wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi iliyofanyika katika kituo hicho, ambapo moja ya malengo ya ziara ilikuwa ni kukagua mifumo ya ukusanyaji wa mapato na hali ya utoaji wa huduma za afya kwa ujumla wake.

“Imarisheni mfumo wa ukusanayaji mapato nataka wakati ujao mapato yaongezeke mara mbili ya sasa, mkumbuke kuwa kwa kadri tunavyodhibiti upotevu wa mapato ndiyo tutakavyoboresha utoaji wa huduma; tutaweza kununua dawa na kufanya maendeleo ya kituo chetu hali itakayochangia kuongeza ufanisi katika huduma zinazotolewa kwa wananchi,” alisema Kulemba.

Ameongeza kuwa Uongozi wa Kituo hicho unapaswa kuhakikisha kuwa mfumo wa GoT-HOMIS unaohusika na usimamizi na uendeshaji wa vituo vya kutolea huduma za afya unafungwa na kufanya kazi kituoni hapo, ili kudhibiti aina yoyote ya upotevu wa mapato kwa kuwa taarifa ya kila huduma na mapato zitaingizwa katika mfumo huo.

Naye Afisa Afya kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema pamoja na kuimarisha mfumo wa mapato uongozi huo uboreshe mazingira kwa kusafisha mara kwa mara maeneo ya kituo hicho pamoja na kupanda bustani za maua.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa idara ya afya wilaya ya Busega, Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya amesema watatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na mganga mkuu wa mkoa ili kutimiza azma ya serikali ya kutoa huduma zinazotakiwa kwa wananchi na kwa wakati.

Baadhi ya wananchi waliopata huduma za matibabu katika kituo cha afya Lukungu wameupongeza uongozi wa kituo kwa namna ulivyoboresha utoaji wa huduma na kuomba hali ya upatikanaji wa dawa iimarishwe zaidi na miundombinu ya kutoa huduma ikiwemo huduma za upasuaji, wodi za kulaza wagonjwa ziongezwe  ili wapate huduma zote kituoni hapo.

“ Kwa upande wa huduma mimi nimehudumiwa vizuri, nimepokelewa vizuri na wauguzi wamenisikiliza baada ya kunisikiliza nimeenda kwenye vipimo na nilivyorudi kwa daktari amenieleza tatizo langu akaniandikia dawa,  nashukuru dawa zote nilizoandikiwa nimepewa,” Mandege William Manyama, mkazi wa Kijiji cha Lukungu.

“Huduma zote nilizokuwa nazihitahitaji nimezipata na nimehudumiwa ndani ya muda mfupi, ombi langu serikali ione namna ya kuongeza huduma hasa za kulaza wagonjwa ili tuipate hapa hapa badala ya kupelekwa kwenye vituo vingine na hospitali,” alisema Daud Moshi mkazi wa Kijiji cha Lukungu.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/09/kituo-cha-afya-lukungu-chatakiwa.html

 

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa