Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali ameweka Jiwe la Msingi katika Madarasa sita ya Shule ya Sekondari tarajiwa ya Dkt. Yohana Balele iliyopo Majahida Mjini Bariadi, ambayo kikamilika kwake kutawapunguzia wanafunzi wa Kata ya Isanga kutembea Mwendo mrefu ambapo sasa wanasoma katika Shule za Sekondari Biashara Kata ya Sima na Kidinda Kata ya Bariadi.
Awali akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, Ndg. Mzee Mkongea Ali, Mwenyekiti wa Mtaa wa Majahida, Ndimi Silanga amesema vyumba hivyo vimejengwa kwa gahrama ya shilingi milioni 97 ikiwa ni michango ya wananchi, wadau mbalimbali wa elimu pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhe. Andrew Chenge.
Kwa upannde wake Elizabeth Jailo ambaye ni mkazi wa Majahida na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Biashara amesema kujengwa kwa shule hiyo kutasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madarasa katika shule anayosoma maana wanafunzi wa shule hiyo wanaotoka karibu na Shule mpya watasoma hapo na kupunguziwa adha ya kutembea takribani kilometa 15 kwa siku.
Pamoja na kuweka Jiwe la Msingi Madarasa hayo, Mwenge wa Uhuru umepitia miradi mbalimbali ikiwepo kufungua Nyumba ya Kulala wageni Nghunde Classic Lodge, kuona mradi wa Uhifadhi wa Mazingira wa Msitu wa Kanisa Katoliki Old Maswa Sesele.
Aidha,umefungua jengo la Wodi ya Wazazi Zahanati ya Mwakibuga na kuona shughuli za wanawake Wajasiriamali pamoja na kuzindua klabu ya kupinga rushwa na klabu ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya shule ya Sekondari Kusekwa.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/05/kiongozi-wa-mbio-za-mwenge-wa-uhuru.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa