• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Kidato cha Nne Simiyu Kuanza Kambi za Kitaaluma Oktoba 30

Posted on: October 22nd, 2020

Wanafunzi wa Kidato cha nne mkoani Simiyu wanatarajia kuanza kambi za kitaaluma tarehe 30 Oktoba 2020, kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa Taifa unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 23 Novemba 2020 hadi tarehe  11 Desemba, 2020.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akizungumza na Maafisa Elimu, wakuu wa shule na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne baada ya kufunga kikao maalum cha kutangaza na kutathmini  matokeo ya Mtihani wa Utimilifu (Mock)  kilichofanyika jana Mjini Bariadi.

Mtaka amesema wanafunzi wote wa kidato cha nne waliopata daraja la I (division one) daraja la IV (division four), daraja la sifuri (division zero) katika Mtihani wa Mock mwaka 2020 na wale wanaotoka katika shule zenye watahiniwa  pungufu ya 30 Serikali imeandaa utaratibu kwa ajili yao, hivyo tarehe 30 Oktoba wanapaswa kufika katika vituo vilivyoandaliwa ambavyo ni Shule ya Sekondari Simiyu na Shule ya Msingi Ndekeja.

“Mwaka huu kumekuwa na majanga  mengi ya moto, majanga ya moto dawa yake si kufunga kambi za shule na ndiyo maana shule za bweni hazijafungwa, tumekuwa na utaratibu wa kambi za kitaaluma kwa watoto wote wa kidato cha nne wa Mkoa wa Simiyu wa shule za Serikali; maelekezo yangu, kambi za kitaaluma kwenye maandalizi ya kidato cha nne zianze na ziendelee mpaka tutakapoanza mtihani wa Taifa,” alisema Mtaka.

Mtaka amezitaka Kamati za Ulinzi na Usalama za wilaya zote mkoani Simiyu kuendelea kuchukua tahadhari na kinga zote za majanga ya moto, huku akibainisha kuwa elimu ya tahadhari ya majanga ya moto imeshatolewa katika shule zote na vifaa vya kuzimia moto vimefungwa  katika baadhi ya shule ikiwemo shule ya Sekondari Simiyu ambacho ni kituo cha kambi hizo.

Akizungumzia suala la motisha kwa walimu na wanafunzi watakaofanya vizuri katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne amesema mwalimu atapewa shilingi 30,000/= kwa kila alama A itakayopatikana kwenye somo lake na shilingi 10,000/= kwa alama B.

Ameongeza kuwa mwanafunzi atakayepata daraja la kwanza pointi saba atapewa shilingi 1,000,000/= na ikiwa atakuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora Kitaifa ataongezewa shilingi 1,000,000/=na kumfanya apate shilingi 2,000,000/=, ambapo amesisitiza kuwa mwanafunzi wa kike atakayefanya vizuri kuliko wenzake wote atapewa shilingi 500,000/= na ikitokea msichana aliyeongoza amepata daraja la kwanza pointi saba atapewa shilingi 1,500,000/=

Shule ya Serikali ya Sekondari ya Mkoa wa Simiyu itakayoingia katika shule 10 bora Kitaifa itapewa zawadi ya shilingi 5,000,000/= huku akiahidi kuwapeleka walimu wote ambao Halmashauri yao itafanya vizuri na kuingia katika nafasi kumi bora Kitaifa kwenda kufanya utalii wa ndani katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu Mw. Ernest Hinju amesema katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2019 Simiyu ilishika nafasi ya tano Kitaifa na matarajio ya mwaka huu ni kushika nafasi ya kwanza Kitaifa, huku akibainisha kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na wazazi wamehamasika kuwachangia wanafunzi chakula.

Kwa upande wao walimu na wanafunzi wameshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kuruhusu kambi za kitaaluma kwa kuwa kambi hizo zimekuwa msaada sana kwa wanafunzi hususani wale ambao wanatoka katika mazingira magumu ambayo hawawezi kujisomea kwa uhuru.

“Awali tuliposikia kambi zimeahirishwa tulisononeka sana maana kambi zimekuwa msaada hasa kwa watoto wanaotoka katika mazingira magumu, hata walimu tunabadilishana utaalamu na mbinu za ufundishaji; tunamshukuru Mhe.RC kuruhusu kambi maana miaka ya nyuma Simiyu ilikuwa nyuma sana kwa ufaulu; lakini sasa hivi tumetoka huko tumepanda mfano matokeo ya kidato cha sita mwaka huu tumeshika nafasi ya tatu na kidato cha nne mwaka 2019 tulishika nafasi ya tano Kitaifa,” Mwl. Khamis Lubugwa.

“Kambi za kitaaluma zimekuwa na msaada sana hususani kwa watoto wa kike, tunapokuwa kambi tunapata muda mwingi wa kujisomea kuliko tunapokuwa nyumbani lakini vile vile tunapokuwa kambi inatusaidia kuepukana na vishawishi mbalimbali maana miongoni mwetu wako wanaotoka mbali, tumejisikia vizuri kufunguliwa kwa kambi na tunatarajia kufanya vizuri sana,” Nshoma Joseph mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Bariadi.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/10/kidato-cha-nne-simiyu-kuanza-kambi-za.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa