Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani TUGHE Simiyu Yatoa Msaada Kituo Cha Afya Ikindilo
Sherehe ya siku wa Wanawake duniani, huadhimishwa kila tarehe nane ya mwezi wa tatu. Katika kuadhimisha sherehe hizo, 2022, kama ilivyo ada Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE-Simiyu), waliamua kufanya matendo ya huruma Wilayani Itilima ambapo ndipo sherehe za siku ya mwanamke kimkoa zimefanyika..
Akiwakaribisha wilayani Itilima Mkurugenzi wa Wilaya ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo amesema ‘’ninafuraha kubwa niwakaribishe sana Wilaya ya Itilima, Pongezi sana Kwa Mwenyekiti na katibu wa TUGHE.Niwaombee baraza za mwenyezi Mungu, niwatie moyo wanawake wenzangu, sisi tunaweza, na tumejionea wazi kabisa kutoka kwa Rais wetu ambaye ni mwanamama Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwanikwa ITILima tu ametupatia fedha mabazo zimewezesha ujenzi wa vyumba 82 vya madarasa. Hivyo wakina mama sote tuwe na moyo wa kumuunga mkono mama Samia Suluhu Hassan, tupambane wenyewe, kila mmoja katika nafasi aliyopewa akaonyeshe uwezo wake. Wakina mama tuendelee kuwashauri kina mama wengine, binti zetu, familia, watoto na Taifa letu, kwani wakina mama ni jeshi kubwa’’.
Akielezea sababu za TUGHE-Simiyu, kuchagua eneo hilo na kufanya matendo ya huruma, Mwenyekiti kamati za Wanawake TUGHE Mkoa wa Simiyu,Bi.Elizabeth Nangali Gelege amesema “ tumeamua kufanya haya matendo ya huruma katika kituo cha afya cha Ikindilo baada ya kufahamishwa na Mganga Mkuu wilaya ya Itilima Dkt. Anorld Musiba. Kuwa kituo cha afya Ikindilo kina mahitaji. Tumekuja na mashuka, mama Samia Suluhu Hassan ameleta majengo, sisi tumeleta sabuni pamoja na mashuka vyote vikiwa na thamani ya Tsh. Milioni moja. Akizungumzia kauli mbiu ya mwaka mhuu ya siku ya wanwake duniani, ambayo inasema:“Kizazi cha Haki na Usawa Kwa Maendeleo, Tujitokeze Kuhesabiwa’’. Bi. Geleje amesema Kauli mbiu hii inaonyesha wazi kwamba huu pia ni mwaka wa sensa, hivyo wanawake tujitokeze kuhesabiwa.Kila mwanamke atumie kipaji chake kuhakikisha watu wa famia yake wanahesabiwa na kuendeleza nchi
Akizungumzia msaada huo Katibu wa TUGHE Mkoa wa Simiyu Bi.Catherine Nyingi amesema katika kuonyesha mshikamano,sisi TUGHE tuna kawaida ya kufanya matendo ya huruma na kurudisha huduma katika jamii.
Akitoa taarifa kuhusu kituo cha afya Ikindilo, Mganga mfawidhi Kituo cha afya Ikindilo Dkt. Elizabeth Malunde amesema Kituo cha afya Ikindilo ni kimoja kati ya vituo 3 vya afya Wilayani itilima. Kituo hiki kimepanda kutoka namba mbili na sasa kipo namba tatu. Kituo cha afya Ikindilo kinatoa huduma mbalimbali kama vile chanjo cha UVIKO,Kliniki ya HIV, tuanafanya tohara kwa watoto wa kiume, wangonjwa wan je na ndani, huduma za mama na motto. Mwaka jana mwezi wa saba tulifungiwa mfumo wa GhoTomis. Upatikanaji wa Dawa 100%, upatikanaji wa damu 100% pia tuna duka la Dawa. Pamoja na mafaniko tajwa hapo juu bado tunakabiliwa na mbalimbali.Changamoto kubwa tuliyo nayo ni kuwa hatuna eneo ila tupo kwenye mchakato wa kutafuta eneo . Pia tuna changamoto ya nyumba za watumishi kwani tuna Nyumba 6 tu na hivyo kufanya watumishi wengine kuishi katika maeneo ya mbali, uchakavu wa majengo, tuna changamoto ya jengo la kulaza wagonjwa- OPD, Changamoto ya watumishi, kituo hakina uzio na hivyo kufanya wanyama kuingia ndani ya eneo la kituo cha afya,pia hakuna wodi ya kulaza watoto wachanga.Mwisho.
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa