• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

RAS SIMIYU Asaini Mikataba ya Miradi Nane ya Ujenzi yenye Thamani ya shilingi 3,219,429,243.

Posted on: May 4th, 2017

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini leo amesaini mikataba ya ujenzi wa miradi nane yenye thamani ya shilingi 3,219,429,243.00  itakayojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) kupitia Kikosi chake cha Ujenzi  (Building Brigade) katika makao Makuu ya Mkoa Mjini Bariadi, Wilaya ya Busega na Itilima.

Mikataba iliyosainiwa ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje la Hospitali ya Mkoa(OPD) litakalojengwa  kwa gharama ya shilingi 1,191,721,678.00, Nyumba ya Mkuu wa Mkoa (shilingi 273,390,082.99), Nyumba ya Katibu Tawala Mkoa(shilingi 266,269,130.29), Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima (shilingi 141,196,144.51) na Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Busega (shilingi 238,061,242.06).

Mikataba mingine ni ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega litakalojengwa kwa shilingi  1, 390,030,338.57, ukamilishaji wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa kwa shilingi 128,247,283.79 pamoja na Ujenzi wa Nyumba 10 za Makatibu Tawala Wasaidizi wa Sekretarieti ya Mkoa kwa gharama ya shilingi 841,540,642.50, ambapo kwa sasa mradi huu utaanza na ujenzi wa nyumba tatu.

Akizungumza na wataalam kutoka Wakala wa Majengo(TBA) na Makao Makuu na Mkoa wa Simiyu kabla ya kusaini mikataba hiyo, Sagini amewataka wataalam hao kuhakikisha majengo yote yanajengwa kwa ubora na kwa muda uliowekwa katika mikataba hiyo.

Meneja wa Kikosi cha Ujenzi cha TBA, Humphrey Killo amesema kikosi hicho kitajenga majengo yote kwa ubora unaotakiwa na ndani ya muda ulipoangwa kwa kuwa kushindwa kuzingatia muda kutawaongezea gharama ambazo hazipo kwenye mikataba.

Aidha, Killo amesema katika gharama za ujenzi wa majengo hayo watazingatia bajeti waliyokubaliana na mteja wao ambaye ni Katibu Tawala Mkoa na kutakuwa na timu itakayofuatilia matumizi ya fedha katika kila kazi itakayofanyika kwa kuwa wana viwango vya chini ikilinganishwa na wakandarasi wengine.

Ukamilishaji wa ujenzi wa miradi hii unatofautiana kulingana na mikataba iliyowekwa kuanzia leo tarehe 04/05/2017 ambapo Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje la Hospitali ya Mkoa(OPD) litajengwa katika kipindi cha miezi sita(06), Nyumba ya Mkuu wa Mkoa miezi sita(06), Nyumba ya Katibu Tawala Mkoa miezi sita(06), Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima miezi minne(04), Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Busega miezi mitano (05), Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega miezi sita(06) ,ukamilishaji wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa miezi miwili (02) na Nyumba 10 za Makatibu Tawala Wasaidizi wa Sekretarieti ya Mkoa miezi sita (06).

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa