• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Katibu Mtendaji NECTA Awaasa Kidato cha Sita Kutojihusha na Udanganyifu Mtihani wa Taifa

Posted on: April 26th, 2019

Katibu MTENDAJI wa Baraza la Taifa la Mitihani nchini (NECTA) amewataka wanafunzi wa kidato cha sita nchini wanaotarajia kufanya mtihani wao wa mwisho mapema mwezi Mei, 2019 kuepuka aina yoyote ya udanganyifu kwenye mtihani huo.

Dkt. Msonde ameyasema hayo wakati akiongea na wanafunzi wa kidato cha sita mkoani Simiyu waliopo kwenye kambi ya kitaaluma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, ambayo inayohusisha wanafunzi 1166 kutoka shule 12 zikiwemo 10 za umma na mbili za binafsi zenye kidato cha sita.

"Niwatake msifanye asilani habari yoyote ya udanganyifu kwenye mtihani wenu, mkifanya hayo tu kwanza yatawafanya mshindwe lakini pili tutakaponusa tu harufu yoyote ya udanganyifu tutawafutia matokeo"alisema Dkt. Msonde.

Wakati huo huo Dot. msonde amewataka wanafunzi hao kuondokana na dhana kwamba mtihani wa Taifa ni mgumu hali inayopelekea kuwa na homa ya mtihani(hofu), badala yake wajiamini na wajiandae vema kwa kuzingatia waliyofundishwa na walimu wao.

Pamoja na hayo amewapongeza viongozi wa mkoa wa Simiyu kwa ubunifu wao wa kuanzisha kambi za kitaaluma hatua inayopelekea mkoa huo kupiga hatua ya katika ufaulu wa mitihani ya kidato cha sita na kidato cha nne.

Awali akimkaribisha Katibu Mtendaji wa NECTA,  Afisa Elimu mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema kuwa awali mkoa ulikuwa na ufaulu mbaya lakini kupitia kambi ufaulu umepanda kuanzia matokeo ya kidato cha sita kutoka nafasi ya 26 mwaka 2017 hadi nafasi ya 10 mwaka 2018 na kidato cha nne kutoka nafasi ya 11 mwaka 2017 hadi nafasi ya 9 mwaka 2018.

Akiongea kwa niaba ya walimu mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Maswa Mwl. Kuyunga Jackson amesema kuwa vijana wa kidato cha sita Simiyu wamepikwa vizuri kitaaluma hivyo matarajio yao ni kuingia tatu bora kitaifa.

Katika hatua nyingine wanafunzi waliopo kambini hapo wamesema kuwa ujio wa katibu mtendaji NECTA umekuwa chachu ya ufaulu wao na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote aliyoyaeleza ikiwemo kuepuka udanganyifu pamoja na kuondoa homa ya mtihani.

"Tunakushukuru Sana kwa ujio wako umetujenga na kutuondolea hofu ya mtihani, tutafanyia kazi uliyotueleza, tunakuhakikishia hatutajihusisha na udanganyifu wowote kwa sababu walimu wametuandaa vizuri na  tunajua udanganyifu unaweza kusababisha tusifikie ndoto zetu; tutazingatia yote tuliyofundishwa na walimu wetu" alisema Julieth John.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/04/katibu-mtendaji-necta-awaasa-kidato-cha.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa