Timu ya wataalam kutoka Mkoa wa Katavi imefanya ziara Agosti 26, 2020 mkoani Simiyu kwa lengo la kujifunza namna kufanya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane) ambayo yamefanyika Kitaifa kwa miaka mitatu mfululizo (2018-2020) mkoani hapa.
Akizungumza na wataalam hao Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amesema ni vema maonesho hayo yakaakisi mahitaji ya wakulima, wafugaji na wavuvi ili kuwasaidia kupata elimu na kuona teknolojia mbalimbali zitakazowawezesha kufanya shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi kwa tija.
Aidha , Bi. Mmbaga ameongeza kuwa ushiriki wa taasisi mbalimbali za Umma na binafsi katika maonesho haya una manufaa kwa wakulima, wafugaji na wavuvi kwa kuwa huwa zinatoa huduma ambazo zinayagusa makundi hayo yote matatu.
"Ili kuboresha Maonesho ya Nanenane suala la uendelevu wa viwanja ni la kulizingatia sana hususani katika dhana ya kutoa elimu kwa wakulima ili waweze kupata elimu ya kilimo bora, wakati wote wanapohitaji kupitia viwanja hivyo," alisema Bi. Mmbaga.
Pichani ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza na wataalam hao na akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ziara hiyo.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-http://simiyuregion.blogspot.com/2020/08/blog-post_66.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa