• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Kambi ya Kitaaluma kwa Wanafunzi wa Kidato cha Nne Wenye Ufaulu Hafifu Yazinduliwa Simiyu

Posted on: September 6th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amezindua rasmi kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu (daraja sifuri) katika mtihani wa ‘Mock’, lengo likiwa ni kuwasaidia waweze kuongeza ufaulu wao katika mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Novemba 2019.

Akizindua kambi hiyo Septemba 05, 2019 Mtaka amesema wanafunzi hao watafundishwa masomo manne tu ambayo ni Kiswahili, Kiingereza ,Uraia(Civics) na Historia, hivyo akatoa wito kwa walimu mahiri waliochaguliwa kuwafundisha wanafunzi hao kwa moyo na upendo ili wanafunzi hao waweze kupata alama D na kuendelea katika mtihani wa Taifa.

“Hawa watoto wafundisheni masomo manne, Kiswahili, Kiingereza, Historia na Civics; wafundisheni kwa moyo, wapeni mazoezi ya mara kwa mara katika siku hizi 60 watakazokuwa kambini, muwasaidie watoke kwenye F wapate angalau D nao wapate vyeti, kwa sababu hata ajira siku hizi kigezo ni angalau mtu awe na cheti cha kidato cha nne” alisema Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa jamii ya Simiyu kuendelea kuwekeza kwenye elimu ili kuuwezesha mkoa kushindana kiuchumi kwa kuwa maendeleo ya kiuchumi yanategemea maendeleo ya elimu katika eneo husika.

Afisa Elimu mkoa wa Simiyu, Mwl.Ernest Hinju amesema kati ya Wanafunzi 9956 waliofanya mtihani wa  Utimilifu (Mock), 1300 hawakupata alama D hata moja, hivyo waliopata matokeo hafifu (daraja sifuri) wamewekwa pamoja wafundishwe masomo manne ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa, huku waliopata daraja la kwanza hadi la nne wakiendelea na kambi kufundishwa masomo yote.

Aidha, Hinju ameongeza kuwa  kambi za kitaaluma zimechangia kuongeza ufaulu kwenye Mtihani ya Taifa wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita, ambapo katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ufaulu ulikuwa asilimia 74 mkoa ukiwa nafasi ya 14 kati ya mikoa 26, mwaka  2017 ufaulu asilimia 79.8 nafasi ya 11 na mwaka 2018 ufaulu asilimia 82.5  ukashika nafasi ya 9 kati ya mikoa 26.

Kwa upande wao wanafunzi wa kidato cha nne waliopo kambini  wameshukuru kuwekewa kambi hiyo na wakaeleza imani yao juu ya uwepo wa kambi hiyo ambapo wameomba kambi za kitaaluma Simiyu ziwe endelevu ili ziwasaidie kujifunza na kujiandaa vema na mitihani ya Taifa hatimaye mkoa uweze kufanya vizuri.

“Tunawashukuru viongozi wetu na wazazi wetu kwa kukubali kutuwekea kambi ya kitaaluma, ninashauri kambi hizi zisiishie kwetu ziendelee na kwa wadogo zetu ili mkoa wetu uweze kuongeza ufaulu” alisema Esther Nashoni mwanafunzi shule ya sekondari Bariadi(Bariadi)

Mkuu wa Shule ya Sekondari Simiyu, Mwl.Paul Susu amesema walimu wamejiandaa vema katika kuwafundisha wanafunzi na kuwapa mitihani ya mara kwa mara ili waweze kufanya vizuri, huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali wa elimu kujitolea katika ujenzi wa miundombinu ya elimu ili kuwe na miundombinu ya kutosha itakayoongeza nafasi kwa kambi za kitaaluma kufanyika  vizuri.

Kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha nne iliyozinduliwa Septemba 05, 2019 ilianza rasmi Septemba Mosi na inatarajiwa kufanyika ndani ya siku 60 kabla ya kufanya Mtihani wa Taifa mwezi Novemba.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/09/kambi-ya-kitaaluma-kwa-wanafunzi-wa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa