Na:IO Simiyu
Kambi Maalumu ya Madaktari Bingwa kutoka Hospitali za Rufaa za Sekou Toure Geita,Musoma,Shinyanga,Simiyu,Kagera na Hospitali ya Kanda Bugando wataweka kambi Mkoani Simiyu ili kutoa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt Yahaya Nawanda ameeleza.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt.Yahaya Nawanda amesema Kambi hiyo maalumu ya matibabu ya madaktari bingwa itaanza kutoa huduma hizo kuanzia Tarehe 12 hadi Tarehe 16 Juni 2023.
Amezitaja huduma zitakazotolewa na Madaktari Bingwa hao kuwa ni pamoja na Uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kama vile Magonjwa ya Wanawake na Uzazi,Magonjwa ya watoto,Upasuaji,Mifupa,Mfumo wa Mkojo,Mionzi,Magonjwa ya Akili,Magonjwa ya ndani kama vile Moyo,Kisukari,Figo,Macho,Presha,pamoja na magonjwa ya Pua,Masikio,na Koo.
Aidha Dkt.Nawanda amemshukuru Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali watanzania kutokana na maboresho makubwa yanayofanyika katika Sekta ya Afya ambapo ametoa rai kwa wananchi kutumia fursa hiyo muhimu kwa kupata huduma hizo muhimu.
Amesema ni muhimu kwa Wananchi kutumia fursa hiyo kwa kuwa hujitokeza mara chache hivyo ni muhimu kujitokeza kwa ajili ya kufanya vipimo na kuzungumza na maktari bingwa hao kwa ajili ya
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa