Kamati yaUshauri ya Mkoa wa Simiyu imeridhia kata za Itubukilo na Sakwe kutokaHalmashauri ya Wilaya ya Bariadi kuhamishiwa Halmashauri ya Mji wa Bariadi naKijiji cha Giriku kutoka Halmashauri ya Mji wa Bariadi kuhamishiwa Halmashauriya Wilaya ya Itilima ili kuwarahisishia wananchi upatikanaji wa huduma karibuna makao makuu ya Halmashauri hizo.
Maamuzihaya ni utekelezaji wa maagizo ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ambayo yalitolewa kwaHalmashauri zote nchini kuhamisha Kata navijiji ambavyo wananchi wake wanavuka makao makuu ya Halmashauri moja kwendakupata huduma katika makao makuu ya Halmashauri zao ili kurahisisha upatikanajiwa huduma.
Akifunguakikao hicho Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) na Mkuu wa Mkoa waSimiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema RCC imefikia maamuzi haya baada ya kupokeamapendekezo ambayo yamefikiwa katika vikao halali vya Halmashauri na kamati zaushauri za wilaya (DCC).
Aidha,katika kikao hicho mwakilishi wa Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mijini naVijijini (TARURA), amesema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 wakala huoumetenga fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Barabara zinazounganishaKata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na makao makuu ya Halmashaurihiyo yaliyopo kata ya Dutwa..
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/04/kamati-ya-ushauri-ya-mkoa-simiyu.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa