• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

JPM Amuagiza Waziri wa Ujenzi Kutafuta Mkandarasi Ujenzi wa Barabara ya Lami Meatu Simiyu

Posted on: September 9th, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasilianona Uchukuzi kutafuta Mkandarasi wa Ujenzi wa barabara za lami (kilomita tatu ) katika Mji wa Mwanhuzi wilayani Meatu Mkoani Simiyu.

Mhe. Rais Magufuli ameyasema hayo Septemba 09, 2018 wakati akiwahutubia wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Stendi ya Mwanhuzi wilayani Itilima mkoani Simiyu, wakati akiwa katika ziara yake  mkoani humo.

Amesema wakati akiwa Waziri wa ujenzi aliahidi ujenzi wa barabara hiyo Waziri wa ujenzi Mawasiliano na uchukuzi ahakikishe anamtafuta Mkandarasi ili aanze kufanya kazi hiyo mwezi huu Septemba 2018, ili ahadi hiyo aliyoitoa kwa wananchi wa Meatu itimie.

“Wakati nilipokuja hapa nikiwa Waziri wa Ujenzi niliahidi ujenzi wa kilomita tatu za lami, nimeshaangaa sana kuona hizo kilomita hazijajengwa, nakuagiaza Waziri wa Ujenzi kabla mwezi huu haujaisha nimuone mkandarasi anaanza kufanya kazi hapa” alisema

Aidha, Mhe. Rais amewataka wananchi kushirikiana na viongozi wao katika kujiletea maendeleo huku akiwasisitiza kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake wazingatie sheria za nchi.

Katika hatua nyingine Mhe. Rais Magufuli amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuweka mipango itakayowezesha wakulima na wafugaji wanafanya shughuli zao kwa amani.

Awali akitoa salamu za Mkoa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa huo una mpango wa kutambua na kuyapima maeneo ya Wafugaji na kuyawekea miundombinu ili wafugaji waachane na ufugaji waachane na kuhama hama na wafuge kwa tija.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi amesema Serikali inajiandaakufanya usanifu wa awali wa Ujenzi wa barabara ya Bariadi-Itilima-Kisesa-Mwandoya-Ng’oboko-Sibiti  ili kwa baadaye ijengwe katika kiwango cha lami.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anaendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani Simiyu, ambapo Septemba 10 amesalimia wananchi katika maeneo mbalimbali ikiwemo Lagangabilili Itilima, Kisesa, Mwandoya, mkutano wa hadhara Mwanhuzi na kufungua majengo ya uboreshaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu, kwa niaba ya vituo vingine 39.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/09/jpm-amuagizawaziri-wa-ujenzi-kutafuta.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa