• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Jenerali Mabeyo Atoa Wito kwa Viongozi wa Dini Kuhubiri Amani

Posted on: December 27th, 2018

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo ametoa wito kwa Viongozi wa Dini nchini kuendelea kuhubiri amani ili kujenga jamii iliyo bora yenye kudumisha upendo na mshikamano.

Jenerali Mabeyo ametoa wito huo wakati wa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro, Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwepo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Benard Kibese na viongozi wengine wa Chama na Serikali, ambapo alisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo kwa Taifa lolote duniani.

"Suala la amani na utulivu ni la msingi sana katika nchi yetu, kwa vile kila mwananchi ana dini yake tunaamini kuwa viongozi wa dini zote kwa kuwa wanasikilizwa sana na waumini wakiweka msisitizo katika suala la amani, amani itatawala na kutakuwa na utulivu"

“Utulivu huu tunauhitaji sana ili tupate maendeleo, kama viongozi wetu wa kisiasa wanavyosisitiza kuwa tudumishe amani na utulivu tupate maendeleo, bila utulivu watu wakiwa wanahaingaika hakuna maendeleo kwa sababu hakuna shughuli mtu anaweza kufanya kama hana amani na utulivu, hivyo hataweza pia kuleta maendeleo yake, familia, jamii na Taifa kwa ujumla" alisema Jenerali Mabeyo

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Simon Sirro amesema vitendo vingi vya uvunjifu wa amani na uhalifu ikiwemo ukataji wa mapanga na mauaji ya vikongwe na yanachangiwa na watu kukosa hofu ya Mungu; hivyo nyumba za ibada(makanisa na misikiti) zinapojengwa kwa wingi zitakuwa msaada mkubwa sana kwa watu kuwa na hofu ya Mungu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema jamii inayoamini uwepo wa Mungu haiwezi kuwa na vitendo vya kisasi, kukatana mapanga na mauaji ya vikongwe huku akiwaasa Watanzania kukaa kwa amani na upendo bila kufanya mambo yanayoweza kuhatarisha amani.

Akibariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro, Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega, Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu amewataka Watanzania kupendana na kuacha roho ya ubinafsi na visasi.

Aidha, Askofu Sangu ametoa wito kwa viongozi na waumini kufanya nyumba za ibada zibaki nyumba za sala kama yanenavyo maandiko matakatifu na kamwe zisitumike kama majukwaa la wanasiasa.

" Palipo na msamaha pana umoja, uelewano na usawa lakini palipo na kisasi hapana maendeleo; nyumba ya ibada isitumike kama jukwaa la Wanasiasa alisisitiza Muhashamu Askofu Sangu.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:https://simiyuregion.blogspot.com/2018/12/jenerali-mabeyo-atoa-wito-kwa-viongozi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa