• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Jamii Yatakiwa Kuacha Imani Potofu Matumizi ya Virutubishi kwa Watoto wa Kike

Posted on: December 21st, 2019

Wito umetolewa kwa jamii kuondokana na mila potofu ya kuwazuia watoto wa kike wenye umri wa kuanzia miaka 10 mpaka 19 kutumia virutubishi vya madini chuma na foliki asidi vinavyotolewa kwa rika hilo kwa ajili ya kuwakinga na upungufu wa damu kwa madai kuwa virutubisho hivyo vibaharibu uzazi jambo ambalo halina ukweli.

Wito huo umetolewa na Afisa Lishe wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Chacha Magige katika kikao cha Kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la AMREF Health Africa kwa kushirikiana na Serikali kilichofanyika jana Mjini Bariadi.

"Baadhi ya wazazi wamekuwa wakizuia watoto wao kupata virutubisho vinavyotolewa shuleni kutokana na imani potofu kwa madai kuwa vinaharibu uzazi; tunaendelea kutoka elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa virutubisho hivi na tunapendekeza masuala ya lishe yajumuishwe katika mitaala ya elimu na itakapobidi kufanyike mabadiliko ya mitaala ili kuongeza uelewa wa masuala haya kwa jamii," alisema Chacha.

Awali akitoa taarifa ya hali ya lishe ya Mkoa, Dkt. Magige amesema utoaji wa huduma kwa watoto wenye utapiamlo umeongezeka kutoka asilimia 14 mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 88.4 Septemba 2019; huku uwekezaji katika utoaji wa elimu ya unasihi wa masuala ya lishe ngazi ya jamii pia ukiongezeka kutoka asilimia 50 mwaka 2017 hadi asilimia 72.2 Septemba 2019.

Kwa upande wake Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Ngulyati wilayani Bariadi, Nyabuho Paschal ambaye pia ni muelimishaji rika, amesisitiza watoto wa kike kuona umuhimu wa kutumia Virutubishi vya Madini Chuma na foliki asidi kwa kuwa vina mchango mkubwa katika rika balehe kwa wasichana na kutosikiliza maneno ya upotoshaji yanayotolewa na baadhi ya wazazi na walezi kuhusu virutubishi hivyo.

Naye Mratibu wa lishe ya Mama, watoto na vijana balehe kutoka Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Bibi. Tufingene Malambugi amesema katika ziara iliyofanywa na Kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start katika vituo vya kutolea huduma za afya wilayani Bariadi, ilibainika kuwa shughuli mbalimbali za afya na lishe zinatolewa  ikiwemo matibabu ya utapiamlo na utoaji wa elimu ya lishe.

Meneja Mradi wa Right Start Initiatives  mikoa ya Simiyu na Mwanza, Dkt. Rita Mutayoba amesema pamoja na shughuli za afya na lishe mradi huu pia unatoa elimu ya lishe ngazi ya jamii kupitia vipeperushi na mabango, kufanya uhamasishaji kupitia wahudumu wa afya ngazi ya jamii, mikutano ya uhamasishaji ya mara kwa mara ambao unafanywa kwa kutumia ngoma za asili ili kufikisha ujumbe katika maeneo husika.

Sanjali na hilo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la AMREF Health Africa, Dkt. Florence Temu amewashukuru wadau wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika utekelezaji wa mradi wa Right Start unaotarajiwa kufikia ukomo  wake mwezi Machi 2020, huku akibainisha kuwa mradi huo umesaidia kuboresha masuala mbalimbali ya afya na lishe.

Wakati huo huo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah Bw. Donatus Weginah amesema Mkoa wa Simiyu utaendelea kuweka mipango madhubuti ya kuendeleza shughuli mbalimbali za masuala ya afya na lishe zinazofanywa na Mradi wa Right Start na kuhakikisha malengo yaliyowekwa ya wananchi kuwa na lishe bora yanafikiwa.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/12/jamii-yatakiwa-kuacha-imani-potofu.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa